Na Magreth Magosso,Kigoma.
WATUMISHI Saba wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoa
wa Kigoma ,wamesimamishwa kazi kwa muda
usiojulikana ,huku watumishi watatu wakikabidhiwa kwa Jeshi la Polisi la mkoani hapo,kwa uchunguzi
wa kina kutokana na tuhuma za upotevu wa
fedha zaidi ya sh.Milioni 960 ambazo zilitengwa kwa ajili ya shughuli za
maendeleo ya wananchi .
Akithibitisha kauli
hiyo jana kigoma Ujjiji, mbele ya Majira
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein Ruhava alisema waliosimamishwa ni
pamoja na watumishi kutoka idara ya Maji,Manunuzi,fedha na uhandisi ambao wameipa sintofahamu manispaa
katika utekekelzaji wa miradi lengwa katika fedha hizo.
Alisema kwa mujibu wa
uchunguzi uliofanywa na mkaguzi wa ndani wa manispaa hiyo na kubarikiwa na
baraza la madiwani walibaini kuchakachuliwa kwa fedha hizo ambapo kiasi cha
milioni 42 zilitengwa kwa ajili ya elimu kupitia mradi wa EQUIP na kuitaka serikali kuu hasa ya serikali ya mtaa na
uongozi wa mkoa kuwashughulikia walengwa
kwa nia ya kuunga mkono jitihada ya serikali ya Tano katika kuwaadhibu
wabadhilifu wa fedha za umma.
Aliyataja majina ya
watuhumiwa hao ni pamoja na Christina Nimaiyunzi ambaye kwa sasa amefutwa
kazi,Malko Maiko ambaye alikuwa mkuu wa idara ya fedha na kwa sasa ameondolewa
katika idara hiyo ,Sultan Ndoliwa ,Fredi Shimba ,Shadrack Baruti na Boniface
Wiliam wamesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi .
Meya huyo alisisitiza
kuwa,Serikali kuu isaidie kumrudisha Kigoma aliyekuwa Mkurugenzi wa hapo
Boniface Nyambele ambaye amehamishiwa kazi mkoani mwanza aje ajibu tuhuma dhidi
ya upotevu wa fedha hizo sanjari na
aliyekuwa Mganga wa manaispaa John
chacha ambaye aliacha kazi kwa hiari hivi karibuni kwa kuwa ni miongoni
wa ubadhilifu wa fedha hizo.
Wakati huohuo Mbunge wa
Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe alishangazwa na hujuma zinazofanywa katika
mradi wa mtaro wa Lubengela kwa kujengwa kinyume cha makubaliano ya mkataba
hasa kutumia malighafi yam awe laini badala yam awe magumu ambayo yanauwezo wa
kuhimili dhoruba za mafuriko katika upitishaji wa maji kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269