DAR ES SALAAM
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipa wiki mbili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU, kuchunguza na kuwafikisha Mahakamani wote waliohusika kula njama ili kiasi cha sh. Bilioni saba zilipwe kwa watu hewa kutipita mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam- DMDP.
Makonda amesema, leo kwamba baada ya kubaini hataachwa yeyote aliyeshiriki kadhia hiyo, kuanzia Mtendaji wa Mtaa mpaka kwenye Ofisi ya Mthamini wa Serikali Mkuu kwa sababu kama uchunguzi wa Ofisi yake usingebaini njama hizo, maana yake serikali ingepoteza fedha na bila shaka fedha wangeliwa na walipanga njama.
Amesema tayari ameshaiandikia barua Takukuru kwa ajili ya utekelezaji wa agizo na kufafanua kuwa Wilaya ya Ilala na Temeke ndizo zimeongoza kwa kukiuka taratibu na kufanya ubadhilifu wa zaidi ya sh. Bilioni tano huku na Kinondoni zaidi ya sh. Bilioni moja.
Makonda amesema kwa upande wa Temeke na Ilala hali hiyo imebainika baada ya kutaka kujiridhisha na kuweka kumbukumbu sawa kabla ya kusaini vitabu kwa ajili ya kupitisha fedha za miradi ya DMDP ambapo baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa vitabu vilivyotakiwa kusainiwa kwa ajili ya kupitishwa fedha kiasi cha sh. Bilioni kumi, vilikuwa 31 lakini ikagundulika kwamba vitabu Vinane vimekiuka taratibu na masharti.
Kuhusu Wilaya ya Kinondoni kiasi hicho cha fedha kilichofanyiwa ubadhilifu kimebainika baada ya uchunguzi kubaini kuwa uthamini umekiuka taratibu kadhaa. Miradi ya DMDP inahusika na ujenzi wa Barabara, Miferreji na uboreshaji wa jiji la Dar es Salaam
UFAFANUZI WA KINA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amefanikiwa kugundua kasoro mbalimbali ambazo zilikuwemo kwenye taarifa za majedwali ya fidia ya waathirika wa miradi ya DMDP inayoendeshwa hapa jijini.
Katika taarifa hizo Mh Paul Makonda amegundua uwepo wa mapungufu mbalimbali katika michakato ya uthamini wa miradi hii ambayo ingeisababishia serikali upotevu wa kiasi cha TSHS 7,581,314,739.
Baadhi ya mapungufu yaliyotajwa na Mh Mkuu wa Mkoa ni kama ifuatavyo.
MIRADI YA DMDP ILALA NA TEMEKE TSHS 5,708, 248,779/=
Mh Mkuu wa Mkoa alipitia zaidi ya vitabu 31 vya fidia za uthamini vya miradi ya DMDP wilaya za ILALA na TEMEKE na kugundua mapungufu yafuatayo.
Kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni mbalimbali kama zilivyoainishwa katika Mwangozo wa Uthamini uliotolewa na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Juni 2015.(ambao tutauita kuanzia sasa Mwongozo).
I) Ukiukwaji wa kifungu 7.1 (10) cha Mwongozo unachotaka
a) Kuwepo kwa picha ya mthaminiwa aliyopigwa katika eneo lengwa linalothaminiwa.
b) Baadhi ya wathaminiwa kutumia picha za pass port size badala ya zile walizopigwa katika maeneo yao yanayolengwa na uthamini.
II) Ukiukwaji wa kifungu 9.1 Sehemu III (iv) ya Mwongozo.
Unaotaka mthamini kuorodhesha majina kamili matatu ya wathaminiwa yatakayotumika wakati wa uthamini na ulipaji wa fidia.
III)Ukiukwaji wa Kifungu 9.2 Sehemu II ya Mwongozo.
Kinacholekeza mthamini kumpa namba kila mthaminiwa ambayo itatumika wakati wa kuandaa taarifa ya malipo.
MRADI WA DMDP KINONDONI. TSH 1,873,065,960/=
Katika taarifa yake hii Mh Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amegundua mapungufu makubwa na ukiukwaji wa kanuni mbalimbali za uthamini kama zilivyoainishwa katika Mwongozo wa Uthamini uliotolewa na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa serikali Juni 2015.
Baadhi ya mapungufu na ukiukwaji huo ni kama ifuatavyo÷
I) kuwepo kwa majina ya wathaminiwa wasiostahili ndani ya orodha ya uthamini wa Mradi wa DMDP Kinondoni.
Majina ya watu au kaya zisizoguswa na mradi wa DMDP kuwepo ndani ya majedwali.
II) Majedwali ya fidia kuwa na kiasi cha fidia inayostahili kulipwa kwa mthaminiwa bila ya kuwepo kwa namba ya uthamini,Jengo wala jina la mthaminiwa.
III) Baadhi ya watu kughushi taarifa za umiliki wa majengo.(Majengo hewa)
IV) Uchanganywaji wa taarifa unaosababisha haki kutokutendeka katika malipo na kuibua malalamiko.
V)Kutokuwepo kwa usawa katika zoezi la uthamini. Mfano Kuthamini baadhi ya makazi kwa kiwango cha thamani kidogo na kuthamini kitu kama shimo la taka kwa thamani ya juu zaidi ya ile ya nyumba.
VI) Kuwepo kwa uthamini usio Stahili.
Mfano kuweka kiwango cha juu ya thamani ya jengo (over pricing) tofauti na uhalisia wa jengo au eneo husika na vice versa.
VII) Majina Yale yale kutumika zaidi ya mara tatu kama vile ni watu watatu tofauti wakati ni mtu mmoja
KATIKA MCHAKATO WA ZABUNI YA UTHAMINI.
Mh Mkuu wa Mkoa amegundua pia kuwepo kwa dosari kubwa sana katika mchakato mzima wa utangazwaji na upatikani wa kampuni stahili ya kufanya uthamini.
Kampuni iliyopatikana imeonekana wazi kuwa si kampuni ya Uthamini bali ni kampuni ya ukandarasi wa mabomba inayojishughulisha na kandarasi za usambazi wa mifumo ya mabomba ya mafuta.
Mh Mkuu wa Mkoa amegundua pia kampuni hiyo ilifanya uvunjifu wa sheria kwa kutoa kazi ya uthamini kwa mtu binafsi ambaye ni mtumishi wa serikali.
Mkuu wa Mkoa amewakabidhi taarifa hizi TAKUKURU na kuwapa muda wa wiki mbili ili waweze kushughulika na mapungufu yaliyogunduliwa awali na kuwafikisha mahakamani watumishi wote na wananchi watakaonekana kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika udanganyifu huo kwa nia ovu ya kuingizia serikali hasara ya bilioni za Kitanzania 7.58
Your Ad Spot
Apr 4, 2017
Home
Unlabelled
MAKONDA KUWAPELEKA MAHAKAMANI WALIOCHAKACHUA MPANGO WA DMDP WAKOMBE SH. BILIONI SABA
MAKONDA KUWAPELEKA MAHAKAMANI WALIOCHAKACHUA MPANGO WA DMDP WAKOMBE SH. BILIONI SABA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269