Daktari
Bingwa aliyebobea katika Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique
Parkar akifanya upasuaji wa kutumia njia ya matudu madogo kwa
kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Baadhi
ya madaktari kutoka katika Hospitali za umma na binafsi nchini
wakifuatilia mubashara upasuaji wa njia ya matundu madogo uliofanyika
leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imendelea kuwajengea uwezo madaktari wa ndani
na nje ya hospitali kwa kufanya upasuaji wa njia ya matundu madogo
(laparoscopic surgery).
Miongoni
mwa madaktari walioshiriki kwenye upasuaji huo ni kutoka hospitali ya
za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan.
Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya
Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha,
Morogoo na Dodoma.
Lengo
ni kuwaongezea ujuzi madaktari hao ili waendelee kufanya upasuaji wa
kutumia njia ya matundu madogo kwa wagonjwa mbalimbali.
Upasuaji
huo unafanywa na madaktari wa muhimbili kwa kushirikiana na Daktari
Bingwa aliyebobea katika magonjwa ya kinamama na uzazi, Profesa Rafique
Parkar ambaye amekuwa akifanya upasuaji huo nchini Afrika Kusini, Kenya
na nchi mbalimbali barani Afrika.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama na Uzazi, Vicenti Tarimo wa hospitali
ya Muhimbili amesema wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji na kwamba
wengine watatu walikuwa wakiendelea kufanyiwa upasuaji huo leo.
“Leo
wagonjwa wenye matatizo ya uzazi na wenye uvimbe wamefanyiwa upasuaji
kwa kutumia njia hii. Kesho wagonjwa wengine watano watafanyiwa upasuaji
kwa kutumia njia hii,” amesema Dk Tarimo.
Dk.
Tarimo amesema lengo ni kuwawezesha madaktari wa hapa nchini kutumia
njia matundu madogo kufanya upasuaji badala ya kutumia njia ya kufungua
tumbo ambayo mgonjwa anatumia muda mrefu kupona.
“Upasuaji
wa njia ya matundu madogo una faida kubwa, kwanza mgonjwa anapona
haraka tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo. Wagonjwa wanaofanyiwa
upasuaji wa njia hii ya kisasa wanaweza kuendelea na kazi kwani baada ya
muda mfupi wanapona,” amesema Dk Tarimo.
Hospitali
ya Muhimbili imekuwa ikifanya upasuajia wa njia ya matundu madogo na
sasa inaongeza uwezo kwa madaktari mbalimbali nchini wakiwamo madaktari
wa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269