Mbunge
wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi akifungua kikao
cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya Kishapu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga
akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati hicho kikao hicho.
Wajumbe
wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo kutoka kushoto, Grace Chamila, Mh. Regina,
Salma Kalebo na Thomas Ng’ombe wakifuatilia kikao hicho.
Mbunge
wa zamani wa Jimbo la Kishapu ambaye ni Diwani wa Kata ya Uchungani
wilayani humo, Paul Makolo akitoa uzoefu wake kuhusu namna ya fedha za
Mfuko wa Jimbo zinavyofanya kazi wakati wa kikao hicho.
Washiriki
wa kikaao hicho wakiwemo madiwani, watendaji kata, vijiji, wenyeviti wa
vijiji, maafisa tarafa na viongozi wakifuatilia kikao hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi (katikati)
akiongoza kikao cha Mfuko wa Jimbo jana. Wengine pichani kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga
na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu, Shija
Ntelezu.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga
akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, Helen Chacha, Diwani wa Kata ya
Uchunga, Paul Makolo na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu
wakifuatilia kikao hicho.
……………………..
Mbunge
wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi amewataka
wananchi kuwa kichocheo cha miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila
kujali msingi ya tofauti zao.
Nchambi
alisema hayo jana wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo
kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo jumla y
ash. Milioni 82 zinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya shughuli za
maendeleo.
Katika
kikao hicho kilichohudhuria pia na madiwani, watendaji mbalimbali na
viongozi wa dini alisema wananchi wanaoibua miradi ya maendeleo na
Serikali kupitia Mfuko wa Jimbo inawapelekea fedha ili zitumike kufanya
miradi hiyo.
Alisema
viongozi wa ngazi za kata wakiwemo madiwani na watendaji wana nafasi ya
kuhamasisha wanancho wao kushiriki katika shughuli za maendeleo na
kutoa elimu kuhusu fedha za mfuko huo.Mbunge huyo alibainisha kuwa
katika mwaka huu fedha zinazotarajiwa kutolewa katika jimbo hilo
zitasaidia katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata
mbalimbali.
Nchambi
alizihakikishiwa taasisi na wananchi kuwa tayari kuwasaidia katika
hatua za kuunganisha umeme lengo likiwa kila mmoja apate huduma hiyo
bila kujali tofauti zao mbalimbali.Kwa mujibu wa mbunge huyo nishati
hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na kuzidi kuimarisha uchumi
kwenye jimbo na pia halmashauri ya wilaya nzima kwa ujumla wake.
“Tumuunge
mkono Rais wetu ana dhamira nzuri na anataka kila mwananchi awe
ameunganishwa umeme kwani umeme utahamasisha maendeleo kwenye jimbo letu
na kata zake, tunataka jimbo liwe na shapu shapu,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Stephen Magoiga aliwataka wanakamati hiyo kuwa makini katika kusimamia
fedha za Mfuko wa Jimbo.Magoiga alisema fedha hizo zinapaswa kufanya
kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwa zinapaswa kusimamiwa
vizuri ili kuendana na kauli mbiu ya Rais ya hapa kazi tu.
Aidha,
alitumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji na wenyeviti wote wa vijiji
kufungua akaunti benki ili kuhifadhi fedha za miradi wanazopokea badala
ya kuhifadhi kwenye akaunti binafsi.
Mkurugenzi
mtendaji aliwataka kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na
kuwa Serikali itawasaidia pale ambapo watakuwa wameibua miradi ikiwemo
kuanzisha majengo ya huduma za kijamii.
Alimpongeza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack kwa kutoa mabati 171 kwa ajili
ya kuezekea vyumba vya madarasa katika shule za msingi akisema kuwa
hatua hiyo itasaidia kujenga Kishapu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269