Kijana
akisukuma tolori huku akipita kwenye matope katika Stendi ya mabasi ya
Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam jana. Watumiaji wa stendi hiyo
wameomba Manispaa ya Temeke kuwawekea miundombinu mizuri ili kuruhusu
maji kupita katika kipindi hiki cha mvua.
Muonekano wa stendi hiyo katika kipindi hiki cha mvua.
Wafanyabiashara wakiendelea na biashara zao kwenye stendi hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATUMIAJI
wa Stendi ya Mabasi ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam wameiomba
Manispaa ya Temeke kuboresha miundombinu ya stendi hiyo katika kipindi
hiki cha mvua ili kuondoa adha wanayokabiliana nayo ya kujaa maji.
Ombi
hilo limetolewa Dar es Salaam jana na wafanyabiashara na madereva
wanaotumia stendi hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu
changamoto hiyo waliyonayo ya kujaa maji hasa katika kipndi hiki cha
mvua za masika.
Mfanyabiashara
ndogo ndogo katika stendi hiyo, Afidh Abdallah alisema katika kipindi
hiki cha mvua stendi hiyo imekuwa ikijaa maji na kusababisha matope
hivyo kuwa kero kwao.
"Mvua ikinyesha hatuwezi kufanya biashara katika stendi hii tunashindwa kuzunguka kufuata wateja" alisema Abdallah.
Abdallah
alisema kwa kutumia fedha wanazolipa ushuru kila siku manispaa hiyo
inaweza kuwawekea hata molamu kwa kipindi hiki cha mvua ili kupunguza
madimbwi ya maji wakati wakisubiri kujenga miundombinu ya kudumu.
Mama
Lishe katika stendi hiyo Mwajabu Mohamed alisema maji yanapo jaa katika
stendi hiyo wateja wao wamekuwa wakishindwa kufika kupata chakula
kutoka maeneo mengine kwa kuhofia madimbwi na matope yanayokuwepo.
Said
Khatibu ambaye ni dereva wa basi la Manshallah linalofanya safari zake
kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini alisema wakati huu wa mvua
changamoto kubwa inayokuwepo eneo hilo ni kushindwa kupata nafasi ya
kupakia na kushusha abiria kutokana na maji yanayojaa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269