Na Magreth Magosso,Bujumbula
MKUU wa Mkoa wa Ruyigi Nchini
Burundi Abdallah Hassan, amewataka warundi wote walioko nje ya Nchi hiyo kwa
madai ya Ukimbizi ,warudi nchini humo,ili kuinua uchumi,umoja na mshikamano wenye
manufaa ya kulijenga taifa hilo.
Akitoa kauli hiyo hivi karibuni
mkoani ruyugi baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo mkoani
Kigoma kuzulu mkoani hapo kama sehemu ya kuimarisha ujirani mwema baina
yao,huku akisisitiza raia wa burundi
waliokimbia machafuko, kwa sasa hawana sababu ya kufanya hivyo, kutokana na
hali ya usalama na utulivu kuimarika kila kukicha na kuwataka warudi ili, kuinua uchumi wao kwa ujumla.
Hassan aliongeza kuwa baada ya
machafuko ya kisiasa ya mwaka 2015, raia wao bado wanakimbia kwa madai ya machafuko
ambayo hivi sasa hayapo na kuwataka kurejea na kuipenda nchi yao kwa kuwa burundi
itajengwa na kulindwa na warundi wenyewe na si watu wengine .
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya
Kibondo Tanzania Luis Bura , aliishauri
Serikali ya Burundi kutengeneza mazingira salama yenye kuhamasisha na kuwarudisha
watu wake nchini mwao, kwa kuwa amani ipo na kuonya warundi wanaokimbia na
kuingia kigoma kupitia kambi za wilaya ya kibondo kuwa,hawana sifa za ukimbiazi.
“katika kujiridhisha na utulivgu
uliopo hapa,kamati ya ulinzi ya wilayani kibondo tumezuia kupokea wakimbizi wasiokidhi sifa ya ukimbizi
na kambi za kibondo hatupokei ,lakini wekeni mazingira rafiki watu wenu warejee
kwa amani” alisisitiza Bura.
Na Jiji la Bujumbula linalodaiwa
kukubwa na machafuko mwaka 2015,lakini
kwa sasa hali shwari wakazi wake wakiendelea na shughuli mbalimbali za
kimaendeleo ambapo Majira ilibahatika kufanya mahojiano na Buchumi Shomari na
Ngenda Banka kwa nyakati tofauti waliwatoa hofu ndugu,jamaa na rafiki zao
waliokimbia warudi kwa kuwa kuna usalama wa kutosha.
Wakati huohuo wakazi wa mkoa wa Ruyigi ambao
wanaishi karibu na Nchi ya Tanzania,
Hamida Kharufan na Didas Luzovil kwa nyakati tofauti walifafanua
kuwa,kilichobaki kwa sasa warundi wengi wanakimbia njaa na kutoa wito kwa
wenzao warudi Burundi wakafanye kazi kwa maslai mapana ya taifa lao
“Sisi hivi sasa nchi nzima ya
Burundi tunasafiri usiku kilometa nyingi bila kubugudhiwa na Mtu yeyote
kutokana na utulivu uliopo sasa, hao wanaoendelea kuitoroka nchi wanakimbia nini warudi tujenge nchi yetu,kwa
kuwa ukimbizi si mzuri ’’alisema Ngenda
Banka.
Majira ilipata fura ya kuzungumza na
Kiongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha CNDD FDD, nchini humo Niyonashima
Desire juu ya kutuhumiwa kuwasambaratisha raia ambao hudai kuwakimbia kwa tabia
ya fujo akana kuwa si kweli ,kwa kuwa wao hawana Jeshi la kuwatisha na kukiri kuwa
kuna wanasiasa wanaowashawishi kutokea kwa fujo zaidi.
Aidha,Nchi ya Burundi iliingia
katika machafuko baada ya Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunziza kutangaza kuwania
muhula wa Pili 2015 na kusababisha warundi wengi kukimbilia katika nchia za
Uganga, Rwanda na Tanzania
.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269