Wananchi
kwa kushirikiana na madereva kuikarabati Barabara itokayo Mbagala Rangi
tatu kwenda kwa Mponda kpitia Vigozi kwa Kashikashi iliyoharibiwa na
mvua zinazo endelea kunyesha na kusababisha adha ya usafiri Dar es
Salaam leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Na Khamisi Mussa,
Mwananchi
aishiye eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Athumani Saidi (a.k.a
John teli), aliseama kero yake ni kuhusu Barabara ni mbovu kupitika na
adha wanaipata na kuomba wahusika kufanyika kazi kero hizi na anahitaji
kujua barabara ipo katika Halmashauri au Manispaa? , na aliseama
Athumani toka kuhamia maeneo hayo anamiaka minne na hajahama na gari
lake kutokana na njia mbovu. akimalizia kusema anaiomba Serikali
kuwatembelea na kusikia kero zao, na mzee Yusufu Ramadhani Nyanza mkazi
wa eneo hilo alikuwa na haya yakusema alisema.
Kubwa
ni Daraja ambapo mvua ikinyesha hakuna wa kuvuka mto mzinga na
kunawanafunzi hushindwa hata kwenda shule kutokana na maji kujaa mto huo na panaumbali wa kilometa kumi na tano hadi kufika shule ya Msingi Mianzini. alisema mzee Ramadhani,
Hospitali hatuna na Kituo cha Polisi kipo Kongowe Mwisho hivyo aliomba huduma za polisi na hospitali wasogezewe karibu, tunakuwa kama watu tuliyosahaulika na wananchi wanazidi kuhamia, alizidi kuiomba serikali kusikia kilio chao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269