Breaking News

Your Ad Spot

Apr 1, 2017

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shamra shamra zikiendelea wakati alipowasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere .
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages