JUMLA ya Pikipiki 14 aina ya
Vespa zenye thamani ya shilingi milioni
37 zimetolewa na Mbuge wa jimbo la Kiwengwa Khamis Mtumwa kwa Makatibu wa
Matawi ya CCM ya jimbo hilo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo huko katika
uwanja wa mpira wa kwa Gube, mbunge huyo alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya
wananchi wa jimbo hilo.
Alieleza kwamba lengo la kutoa
vifaa hivyo ni kuwarahisishia huduma za usafiri
watendaji hao ambao muda mwingi wanakuwa na majukumu mbali mbali
yanayohitaji usafiri wa haraka ili yaweze kutekelezwa kwa wakati.
Aliahidi kuwa hiyo ni sehemu tu
ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jimbo hivyo ataendelea kutatua kero
mbali mbali zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.
“ Nitaendelea kumarisha huduma
mbali mbali za kijamiii kadri mwenyezi mungu atakavyonijaalia, wito wangu kwenu
ni kwamba miradi ambayo kwa sasa naitekeleza katika jimbo hili mnatakiwa
kuitunza ili iweze kuwanufaisha watu wote.”, alisisitiza Khamis.
Akizungumza Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ mara baada ya kukabidhi Pikipiki
hizo kwa watendaji
hao aliwataka viongozi wa majimbo
ya chama hicho kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo
kwa wananchi.
Alisema kwa sasa viongozi
wanatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji
wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015/2020 kwa vitendo ili wananchi waone
maendeleo yanayofanywa na viongozi wao.
Alisisitiza kuwa ni lazima
viongozi wa majimbo waende na wakati Kwa kutangaza na kutoa taarifa za uhakika
juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM , hatua itakayosaidia kujenga imani za
wananchi waliowachagua katika uchaguzi mkuu uliopita.
“ Naendelea kuwakumbusha baadhi
ya wabunge, wawakilishi na madiwani ambao bado utekelezaji wao wa Ilani ya
Chama chetu unasuasua katika majimbo yao kuwa waanze kurudi kwa wananchi
kutekeleza yale waliyowaahidi kabla ya uchaguzi mkuu ujao”, alisema Dkt. Mabodi.
Nao baadhi ya makatibu mbali
mbali waliokabidhiwa vifaa hivyo wameahidi kuvitumia vizuri kwa lengo la
kuimarisha shughuli mbali mbali za chama hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269