Spika Job Ndugai |
Spika wa Bunge Job Yustino Ndugai (Mb), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja
wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge mjini Dodoma, leo, imesema Spika Ndugai amechaguliwa katika uchaguzi ambao umefanyika katika Mkutano wa Maspika wa
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliomalizika leo Mjini Abuja.
Kwa wadhifa huo, Ndugai ataongoza Maspika
wenzake toka Mabunge na Mabaraza ya kutunga Sheria 63 yaliyoko katika
nchi 18 za Jumuiya ya Madola kwenye Bara la Afrika. Wadhifa huo ni wa miaka
miwili kuanzia sasa hadi mwaka 2019 kutakapofanyika uchaguzi mwingine.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mabunge Barani
Afrika ni pamoja na Afrika ya Kusini, Botwana,
Cameroon ,Ghana, Kenya, Lesotho, Msumbiji, Mauritius, Malawi, Nigeria, Namibia,
Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia.
"Kwa hakika nawashukuru
Maspika wenzangu kwa kunipa dhamana hii ya kuwa Mwenyekiti wao, ni heshima
kwangu binafsi lakini zaidi Kwa Tanzania. Ni matumaini yangu kwamba Bunge letu
litaendelea kung'ara kitaifa na kimataifa tukiwa Bunge moja lenye Upendo na
mshikamano". Ndugai amesema baada ya kuchaguliwa kwake.
Huu ni wadhifa wa nne kwa Ndugai katika
masuala ya Bunge kwenye medani ya Kimataifa. Amewahi kuwa Mwakilishi wa Nchi za
Afrika Mashariki katika Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya
Madola Duniani mwaka 2008-2011, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya
Umoja wa Mabunge ya Afrika, Pacific na Carribbean na Jumuiya ya Ulaya mwaka 2011-2014 na Rais wa Baraza la Mabunge
ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC – PF)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269