Mweneyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba
akizungumza na Waandishi wa Habari jana,
jijini Dar es Salaam
|
Baraza Kuu la Uongozi la CUF limewafukuza uanachama wabunge wanane wa viti maalum na madiwani wawili pia wa viti maalum.
Miongoni mwa Wabunge hao wanane, ni pamoja na Kiongozi wa Wabunge wa CUF Riziki Shahali.
Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
Amesema wabunge na madiwani hao wamevuliwa uanachama wao kutokana na kukaidi wito waliopewa na Kamati ya Maadili na Nidhamu ya chama hicho juu ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo kuhusishwa na vitendo ya usaliti ndani ya chama.
Aidha Prof. Lipumba amesema tayari wamemwandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai juu ya maamuzi ya kuwafutia uanachama wabunge na madiwani hao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269