1.Balozi
Dk. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba na Wakili wa serikali ya Brazili Sonia
Nunes, baaya kusaini Mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Serikali ya
Brazil wa Dola Milioni 203 za Kimarekani (sawa na Sh.
Bilioni 443).
--------------
Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Marekani milioni
203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445.
Deni hilo
lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya
Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.
Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dk. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo
kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dk. Sonia Portella Nunes akisaini
kwa niaba ya Serikali ya Brazil.
Kufuatia tukio hilo, Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga
mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa
Tanzania.
Aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania
katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na nchi hiyo.
Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye hafla hiyo Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka
Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya
ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na deni hilo
lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.
Hivyo kutoka sasa kampuni za Brazil zinaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil
kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania
inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.
BaloziDk.
Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya
Brazil.
1BaloziDkt. Emmanuel Nchimbi na Mkuu
wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi)
wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili (Tanzania na
Brazil)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269