NA MWANDISHI MAALUM
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana alifungua
Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja.
Tamasha hilo
lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue ,Jambiani na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali
pamoja na wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa
Rais aliwashukuru Waandaaji wa Tamasha hilo ambao wamesaidia kuwaleta wanawake
wa mkoa wa Kusini pamoja.
Makamu wa
Rais amewapongeza wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kuwa wa kwanza kutekeleza wazo
lililowazwa na kuonyesha utamaduni wa Kusini.
Mhe. Samia
alisema Utamaduni wa zamani hauna budi kuendelezwa ili vijana wa sasa wajue
wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea.
Akivitaja
baadhi ya vitu alivyoviona kwenye ufunguzi huo kama Manda, Mabobwe ,Vipopoo, ngoma
ya Msanja ambavyo kwa pamoja vina lengo la kuleta yale mazuri ya zamani ambayo
yametutoka.
Alisema
Vijana wengi hawajui Kiwe-jiwe la kusagia chakula (Blender za Bibi zetu) wao wanajua Blender, hivyo ni vyema Tamasha
hili likaja na vitu vingi mwakani waelewe hata maji tuliyatunza kwenye Mtungi
ambao wao kwa sasa wanayajua Majokofu.
Hivyo
aliwasihi Wanawake wa kusini kufufua tamaduni zetu na kuzidumisha, alisema sema yeye anatoka Kizimkazi ambapo ngoma
maarufu ni Shomoo na Dandaro.
Makamu wa
Rais alisema kuwa Utamaduni utasaidia kuwafunza watoto wetu uzalendo, mazingira,
nidhamu ya maisha kwani utamaduni
unajumuisha kila kitu kuanzia chakula, mavazi, vifaa vilivyotumika,filamu,
ngoma na burudani mbali mbali.
Mhe. Samia
aliwapongeza sana wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kutoka kwenye utamaduni wa
kukaa tu na badala yake kufanya shughuli zinazowaingizia kipato.
“Nimefurahishwa kuona wakina Mama sasa hivi
wanatoka wana Vikundi vya Kulima tumeonyeshwa wanalima Tungulee, wanalima
Karoti,wanalima michicha hii yote ni utamaduni kwamba tumetoka kwenye utamaduni
wa kukaa tu na kusubiri bwana haji lakini sasa tunatoka tunajituma na sisi
tunapata mapato yetu tunaendelea na maisha yetu”
Makamu wa
Rais alisema ni wajibu wa kila mama kutunza na kufundisha watoto wetu Tamaduni zetu, “Tunautamaduni ambao hautakiwi kuonyeshwa
mbele za watu na ule nao tufundishe watoto wetu, tusiuache , tunakuwa wa kisasa
mno, tunajifanya wa kisasa mno kiasi ambacho mambo mengine tunayaacha lakini
ambao kwa sie tuliofanyiwa huko nyuma unajua faida yake na watoto wetu
wanaokosa kufanyiwa sasa hivi tunaona hasara yake”
Makamu wa Rais alitoa rai kwa waandaaji wa Tamasha hilo kuhakikisha linafanyika
kila mwaka na kujumuisha tamaduni mbali mbali zenye lengo la kujenga na
kuimarisha mshikamano pamoja na kudumisha upendo na amani katika jamii,
aliwashukuru wadhamini waliosaidia kufanikisha
Tamasha hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioniMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni
Wasanii wa Kikundi cha Majalis Saniya kutoka Michenzani wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wasanii wa Kikundi cha Tausi kutoka Kisiwandui wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Wasanii wa Kikundi cha Tausi kutoka Kisiwandui wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269