Breaking News

Your Ad Spot

Sep 3, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AOMBOLEZA KIFO CHA MUHINGO RWEYEMAMU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ametuma salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa mwandishi wa habari nguli na Mkuu wa Wilaya za Handeni na Morogoro, Muhingo Rweyemamu (Pichani), kilichotokea jana tarehe 2 Septemba, 2017.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Wizara ya habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, imesema Waziri Mwakyembe ameeleza kupokea kwa mshituko na masikitiko taarifa za kifo cha Muhingo ambaye mwezi Juni mwaka huu alikwenda kumjulia hali hospitali ya AgaKhan alipokuwa amelazwa na kuonyesha dalili za matumaini.

"Kifo chake ni pigo kubwa kwa wanatasnia na wadau wa habari wote na wananchi aliowahi kuwaongoza katika uhai wake, naiombea familia ya marehemu, ndugu na maraki waweze kupita kipindi hiki kigumu na Mungu awape nguvu na ujasiri", amesema Dkt. Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages