NA BASHIR NKOROMO
Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa awali.
Wakati katika awamu ya kwanza Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.
Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181. PICHA ZA UCHAGUZI HUO/>BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Sep 25, 2017
Home
Unlabelled
RUTAHINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA
RUTAHINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269