Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga ukuta katika kituo cha afya Mganza Halmashauri ya Wilaya Chato.
--------------
GEITA, TANZANIA
Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Wilayani humo.
--------------
GEITA, TANZANIA
Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Wilayani humo.
Mhandisi Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na wananchi
kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili pamoja na Ofisi
katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la wanafunzi 2,212 kutoka
1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao wanasoma kwa awamu mbili hivyo,
kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 28.
Akizungumza na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa
Serikali inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine kwa
kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na walimu wa
kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na viongozi wote katika
utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo ameshiriki
katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya wananchi kupata huduma
katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na vituo vipya vya afya.
Miradi hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa kujitolea kufanya kazi
hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula wanapokuwa katika eneo la
kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta maji, mchanga, sementi, kokoto na
kushiriki katika ujenzi.
Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa baada
ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina kuhusu mikakati
na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati kwa Wakuu
wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Tarafa, Maafisa elimu wa
Wilaya na Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akichanganya mchanga na simenti
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mganza (Chato) alipofanya ziara
ya kikazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.
Akina
mama wa kijiji cha Ilyamchele Wilayani Chato wakishiriki katika ujenzi
wa vyumba viwili na Ofisi shule ya Msingi Ilyamchele kwa kusogeza
matofali kwa mafundi wa ujenzi.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchimba msingi wa
kujenga vyumba viwili na ofisi na wananchi wa kijiji cha Ilyamchele
(awapo kwenye picha)katika uzinduzi wa kampeni ya kujenga vyumba vya
madarasa na zahanati Wilayani Chato.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Ilyamchele baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na zahanati kijijini hapo.
Mkuu
wa mkoa akizungumza na wanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi
Ilyamchele wakati akikagua shule hiyo ambayo ina madarasa 6 huku darasa
la pili likiwa na wanafunzi 407 wanaosoma kwa awamu mbili.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269