Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akifanya majaribio ya kuchunguza wadudu kwa kutumia hadumini
iliyopo kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa
mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Novemba 18, 2017 jijini Dar es
salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wa kwanza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa
wataalam wa chuo cha Afya na Tiba KAM kuhusu vifaa vinavyotumika maabara
kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya
pili ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa
chuo cha KAM hawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili yaliyofanyika jijini Dar es salaam
Mkurugenzi
wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM Dkt. Aloyce Musika
akizungumza na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha
KAM (hawapo pichani) wakati wa mahafali ya pili ya hicho
yaliyofanyika Novemba 18, 2017 jijini Dar es
salaam.
Baadhi
Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM
wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani
wakati wa mahafali ya pili ya chuo yaliyofanyika jijini
Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha
Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya
afya wakati wa mahafali ya pili ya chuo yaliyofanyika
jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha
Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya
afya wakati wa mahafali ya pili ya yaliyofanyika
jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile kushoto akipokea na zawadio kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo
na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM Dkt. Aloyce Musika kulia wakati wa
mahafali ya pili yaliyofanyika jijini Dar es
salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM
wakimsikiliza wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hicho
yaliyofanyika jijini Dar es salaam. (PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-WIZARA YA
AFYA, WAMJW)
WATUMISHI
wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili
kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili
kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha
Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
“Tuna
malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao
laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado
tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema
Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na
mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani
wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na
mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa
vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumetoa
milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa
milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya
kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba Dkt. Aloyce Musika amesema
kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha
elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa
uhakika nchini.
“Wahitimu
waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa
msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza
ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za
afya kwa uhakika” alisema Dkt. Musika
Mbali
na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni
Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba
Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi
wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa
haraka.
Naibu
Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha
Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya
fani mbalimbali katika kada mbalimbali za sekta ya afya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269