Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania,
Philip Mpango amesema kuwa, ni aibu kuomba misaada nje ya nchi na
kuongeza kwamba, binafsi amechoka kufanya hivyo kwa kuwa kitendo hicho
kinalidhalilisha taifa.
Mpango
aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi, wasimamizi
na wahariri wa takwimu za mapato na matumizi binafsi katika ngazi ya
kijamii. Akizungumzia suala hilo Mpango alisema: Aliweka wazi zaidi
kwamba kuna udharura wa nchi kuwa na mkakati wa kuondokana na hali hiyo
na kwamba, malengo hayo yatafikiwa kama makusanyo ya takwimu yatafanyika
na kutumiwa kwa umakini.
Matamshi ya Waziri wa Fedha wa Tanzania
ya kutofurahishwa na kitendo cha mataifa ya Afrika kuomba misaada kwa
nchi za kigeni, yametolewa katika hali ambayo akthari ya nchi hizo
zimekuwa tegemezi kwa misaada ya wahisani licha ya kuwa na raslimali
nyingi zitokanazo na vyanzo asilia, kama vile dhahabu, mafuta, gesi na
kadhalika. Aidha Rais wa Tanzania John Magufuli naye kwa mara kadhaa
amekuwa akielezea utajiri mkubwa wa taifa hilo hususan madini, lakini
pamoja na hayo bado utajiri huo haujaweza kuwanufaisha Watanzania
kutokana na sababu tofauti kuu zaidi ya yote zikitajwa kuwa ni ufisadi
wa baadhi ya viongozi wasiokuwa na uzalendo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269