Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dk Ali Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kheri James baada ya kushinda katika uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo Cha Mipango mjini Dodoma. wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Tabia Mwita.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita baada ya ushindi wake katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri Denis James akiwa amebebwa na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kutajwa kuwa ndiye Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo kwa miaka mitano
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa UVCCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi katika mkutano huo.
Mara baada ya kutangazwa tu kuwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM),Kher Denis James,kwa furaha kubwa iliyokwenda mpaka kwa Wajumbe wenzake,ilibidi zitumike nguvu za ziada kupunguza vurugu za shangwe zilizotarajiwa kutokea ukumbini hapo,kama uonavyo Mwenyekiti akiwa katika mikono salama ya utuliu akielekezwa kwenda jukwaa kuu.
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya Bi. Tabia Mwita.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa pichani kushoto akitazama tukio la pongezi kutoka Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James.
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt Ali Mohamed Shein akuhutubia wakati akifunga mkutano huo leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa UVCCM Kheri James, nje ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma Desemba 11, 2017 (katikati) ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mh. William Lukuvi ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika uchaguzi wa UVCCM uliofanyika kwenye Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa (Zanzibar),Rais wa Zanzibara Dkt Shein akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiwasili ukumbini
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo leo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakishangilia ukumbini mara baada ya kuwapata viongozi wao katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali.
MATOKEO UCHAGUZI UVCCM TAIFA 2017
1. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Tanzania 2017-2022 ni Ndugu Kheri Denice James.
2. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti...
Kura halali 565
Thabia Mwita 286 (Mshindi)
Rashid Mohamed Rashid 282
#MatokeoUchaguziUVCCM
3. Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara..
Sophia Kizigo
Musa Mwakitinya
Keisha
#MatokeoUchaguziUVCCM
4. Wajumbe 2 kwenda Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Zanzibar..
Abdallaghari Idrisa Juma
Maryam Mohamed Khamis
#MatokeoUchaguziUVCCM
5. Wawakilishi kutoka Tanzania Bara kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa nafasi 3..
Rose Manumba
John Katarahiya
Secky Katuga
#MatokeoUchaguziUVCCM
6. Wawakilishi kutoka Zanzibar kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa
Nasra haji
Abdallah Rajabu
#MatokeoUchaguziUVCCM
7. Mshindi nafasi ya Uwakilishi kutoka Vijana kwenda Jumuiya ya Wazazi ni AMIR MKALIPA
#MatokeoUchaguziUVCCM
8. Mshindi nafasi ya Uwakilishi Vijana kwenda UWT ni DOTO NYIRENDA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269