Naibu
katibu mkuu Tughe Taifa Eng. Amani Msuya (aliye simama) akizungumza
jambo katika hafla fupi ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha
Wafanyakazi (TUGHE), Mkoa wa Dar es Salaam, Mziwanda Chimwege wa kwanza
kulia aliyechaguliwa hivi karibuni baada ya kuwashinda wezake wanne
katika kinyanganyiro hicho, Msuya alisema. anawaomba wanachama kujitoa
kwa hali na mali katika kushirikiana na mwenyekiti wao, kuanzia kushoto
ni Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam, Gaudensi Kadyango na Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Utawala Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Makwaia Makani. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mziwanda Chimwege alianza kwa kumshukuru Mungu pamoja na Mama mzazi na kuwashukuru Wanachama wa Chama hicho kumuamini na kumchagua yeye awe kiongozi wao. na Pongezi maalumu kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) chini ya Uongozi wa Profesa Lawrence Museru
kwa ushirikiano anao upata katika kutekeleza moja ya majukumu yake
katika kujadili na kutatua mambo mbalimbali, Chimwege alisema, anaomba
viongozi na wanachama wampe ushirikiano katika utekelezaji wa kukijenga
Chama ikiwemo kutatua kero mbalimbali ambapo kwanza amesema ataanza na
vipaumbele kama, uwazi na mapato na matumizi ya chama hicho lakini
nikidhani pia shida ya wanachama ni mafunzo kwa viongozi katika ngazi ya matawi na mahitaji ya semina na makongamano kwa wanachama wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam, Tughe kuwa na sacoss ya wanachama |
Mziwanda
Chimwege akimsalimia Mama yake mzazi Fatuma Mziwanda wakati wa hafla
fupi yakupongezwa kwake ambayo iliyoandaliwa na wanachama wa Chama hicho
Chimwenge akisalimia Wanachama kabla ya hafla fupi ya kupongezwa kwake
Mkurugenzi
wa Raslimali Watu na Utawala Hospitali ya Taifa Muhimbili Makwaia
Makani (wa pili kushoto) akizungumza jambo na kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE), Mkoa wa Dar es Salaam, Mziwanda Chimwege,
Naibu katibu mkuu Tughe Taifa Eng. Amani Msuya na
Naibu katibu mkuu Tughe Taifa Eng. Amani Msuya na
Baadhi ya wanachama
Mjumbe
wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Josephine Lwambuka katika
picha ya pamoja na marafiki zake mara baada ya kumpongeza
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269