Breaking News

Your Ad Spot

Dec 11, 2017

TANZANIA YAMKABIDHI BENDERA BALOZI WA UTALII NCHINI MAREKANI

Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory (wa pili toka kushoto) akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Meneja wa Masoko toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena (kushoto) kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani, kulia ni Mwanzilishi wa Kampuni ya Coutious on Tanzania Justa Lujwengana na wa pili kulia ni Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi hiyo Geofrey Tengeneza. Meneja wa Masoko toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory baadhi ya vitabu vinavyoelezea vivutio mbambali vya utalii vilivyopo Tanzania mara baada ya kumkabidhi Bendera ya Taifa kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani. Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory akionesha baadhi ya vitabu vinavyoelezea vivutio mbambali vya utalii vilivyopo Tanzaniakwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa – Maelezo)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages