Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi
ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha
Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana ,
kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo mara
alipowasili katika chuo hicho
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza jambo na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto), wakati mmoja wa
mwanafunzi wa Chuo hicho, Lenah Sauli alipokua akishona nguo
Mkufunzi Mkuu Msaidizi Regina Makotha (kulia) akizungumza kwa kuwapa ishara yale aliyokuwa akizungumza Waziri Mhagama
Wanafunzi
wa Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu
wakiashiria kupiga makofi wakati walipokuwa wakipewa ishara na Mwalimu
wao, Mkufunzi Mkuu Msaidizi Regina Makotha (pichani hayupo) Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao
Balozi
wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza jambo katika
hafla fupi ya kumkabidhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa
pili kushoto) vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni msaada
kutoka serikali ya Kuweit, hafla iliyofanyika jana katika Chuo Cha
Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana,
wakwanza kushoto ni Katibu Muhutasi wa Balozi na wakwanza kulia ni
Mkalimani wa Balozi, Abdallah Yahaya
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cherehani, Lenah Sauli
(kushoto)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimvisha miwani mwanafunzi wa Chuo
hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi umeme
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi
mafuta maalumu ya kujipaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi mwanafunzi wa Chuo hicho, Mandela Lamwai ambaye anasomea ufundi
umeme, wa tatu kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem
KUWAIT YAZINDUA MPANGO KAMILI WA KUWASAIDIA WALEMAVU TANZANIA
Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake nchini umezindua mpango kamili wa kuwasaidia watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Yombo,uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,vijana,Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama,Kaimu wa Chuo Bi Maryam, walimu na wanafunzi wa chuo hiko kilichoanzishwa mwaka 1973 na kutoa mafunzo mbalimbali kama umeme,ushonaji n.k.
Balozi wa Kuwait Al-Najem katika hotuba yake wakati wa uzinduzi amesema kuwa mpango huo utagharimu kiasi cha dola laki 5 sawa na shilingi bilioni 1.1 utaendeshwa nchi nzima kwa awamu kwa kushirikiana na maafisa wa Serikali ya Tanzania na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Pembezoni mwa uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, Al-Najem alimkabidhi Waziri Mhagama vifaa vya walemavu kama viti vya matairi,fimbo,magongo,miwani,vifaa vya kuwasaidia wenye udhaifu wa kusikia na mafuta ya kujipaka kwa walemavu wa ngozi albino huku akiahidi kuchangia vifaa ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa katika Taasisi ya Mifupa MOI.
Kwa upande wake Waziri mwenye dhamana Mhe. MHAGAMA amesema kuwa Tanzania itaendelea kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu walemavu huku akiyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na sekta binafsi kuiga mfano wa Serikali ya Kuwait, watu wake na Ubalozi wake katika kuwasaidia walemavu nchini.
Waziri Mhagama ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa misaada hii na kuuomba Ubalozi kusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili Chuo cha Ufundi Yombo kama vile uchimbaji wa kisima na makazi kwa wanafunzi walemavu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269