Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu ambaye ni raia wa kigeni alipotembelea gereza la Keko jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2018. |
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa
Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah
alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni
sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo.
Mkuu
wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi
Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(hawapo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza
hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza
Keko ambapo chumba hicho kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli
mbalimbali kwa kutumia njia ya TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia
gharama Jeshi la Magereza katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na
kuwarejesha magerezani.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika
Chumba Maalum ambacho kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa
kutumia njia ya TEHAMA(wa kwanza kushoto) ni Kaimu
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
Noel James(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Kiangi Abdallah
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la
Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua
gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika
sekta ya Sheria hapa nchini.(PICHA ZOTE NA JESHI LA MAGEREZA).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269