Breaking News

Your Ad Spot

Dec 23, 2009

SHEREHE YA KUJITATHMINI YA SHIRIKA LA PRINMAT, DAR

KATIBU Mtendaji wa Shirika la Waugunzi na wakunga wa kujitegemea Tanzania (PRINMAT), Keziah Kapesa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kuleimisha dhidiu ya Ukimwi, vijana waliomo katika ndoa, katika sherehe iliyofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Goba, wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, juzi. (Na Mpigapicha Wetu).
KIJANA Mosses Steven  (wapili kuhsoto), akiigiza kuathirika na ukimwi wakati wa sherehe ya kujitathmini ya  PRINMAT katika kuendesha mradi wa kuelimisha dhidi ya ukimwi vijana walio katika ndoa, juzi kwenye kituo cha mradi huo kilichopo Goba, wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam.
 WASANII wa kundi la vijana wa kituo cha elimu ya ukimwi kwavijana walio katika ndoa, kilichopo chini ya PRINMAT cha Goba wilayani Kinondoni, Dar es salaam, wakicheza sindimba wakati wa sherehe hiyo.

STIRY

PTINMAT yapania kupanua wingo mradi uelimishaji vijana walio katika ndoa

SHIRIKA la Wauguzi na Wakunga Tanzania Wakujitegemea (PRINMAT), mwakani litapanua wingo katika mradi wa kuelimisha vijana walio katika ndoa namna ya kujiuepusha na ukimwi.

Hayo yalisemwa juzi, na Katibu Mtendaji wa PRINMAT, Keziah Kapesa katika sherehe ya kutimiza mwaka, mradi wa kituo cha Vijana walio katika ndoa kilichopo, Kata ya Goba, wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema, hadi sasa PRINMAT ambao ni wauguzi na wakunga wanaotoa afya ya uzazi katika maeneo yaliyo mbali na hospitali husa vijijini, ina vituo 58 vya kufunda vijana walio katika ndoa, Dar es Salaam na Morogoro ambavyo ninashughulika na huduma ya mama na mtoto.

Keziah alisema, miongoni mwa vituo hivyo, vitano viko wilaya ya Kinondoni vinavyohusika na mradi wa Ujana na Morogoro vipo vinne vinavyofanya kazi hiyo katika maeneo ya Gairo na Kihonda.

Alisema, katika awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba 2008 hadi Septemba 2009, PRINMAT ililenga kuwafikia vijana 18,000 wa kike wanaofika kwenye huduma za mama na mtoto katika vituo husika na pia kuwaelimisha wanaume vijana waliooa 3,000.

Keziah alisema, lengo hilo lilivukwa na kwa kufikiwa vijana 18,921 wa kike na 14,088 wa kiume. " hawa tuliweza kuwapata kwamafanikio makubwa kutokana na kutumia mbinu nyepesi za kuwavuta na kuwapatia elimu ya kawaida ya malezi ya mama na mtoto na ya kujinga na ukimwi katika ndoa zao"m alisema.

Alisema, PRINMAT imeamua wigo mwaka 2010, kutokana na changamaoto zilizojitokeza katika kutoa kuwahudumia vijana hao ambapo imebainika kuwa mbali na waliomokatika ndoa, vijana wa kawaida nao wameonyesha kutamani kupata huduma hiyo.

Keziah alisema pia wapo ambao wamepata elimu hiyo wakati tayari wameshaathirika na wengine wameandamwa na ulevi wa kupindukia wakiwa ni katika kundi la wenye umri kati ya miaka 15 na 25.


Alisema katika mpango huo, PRINMAT itaanzisha matawikatika maeneo ya mbali na vituo vyake ili kuwafikia vijana wengi zaidi, ambapo katika wilaya ya Kinondoni kutawekwa matawi matatu.


Keziah alisema, PRINMAT inaongeza pia vituo viwili katika maradi mmoja kutoka Berega, Kilosa na mmoja kutoka wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ambapo wanategemea kupata vijana 40,000 kwa mwaka huu wa 2009-2010 ifikapo Septemba 30 kwa jumla vijana wa kike chini ya mradi huo watakuwa 30,000 na wa kiume 40,000.

CIAO































Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages