Breaking News

Your Ad Spot

Jan 28, 2010

JENERALI SARATH FONSEKA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mgombea urais wa Sri Lanka wa upinzani Kamanda wa zamani Jenerali Sarath Fonseka (pichani) amekataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa rais akidai kumefanyika udanganyifu.Katika waraka wake kwa tume ya uchaguzi Jenerali Fonseka amesema atawasilisha malalamiko yake mahakamani, kutaka matokeo hayo yabatilishwe.Ameshutumu rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaska, kwa kutumia vyombo vya habari vya kitaifa kumkashifu, kutumia fedha za umma kufanyia kampeni na kuwazuia Watu aliowategemea kumpa ushindi, wasipige kura.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages