Breaking News

Your Ad Spot

Jan 31, 2010

JERRY MURO MATATANI KWA RUSHWA DAR?

MTANGAZAJI  wa TBC1 Jerry Muro (Pichani) anashikiliwa na katika kituo Kikuu cha Polisi mjini Dar es Salaam, kwa madai ya kukamatwa katika mtego wa kuomba na kupokea rushwa kwa mwananchi mmoja jijini.
Habari za Kipolisi zilizopatikana, zimethibitisha kwamba mtangazaji huyo ambaye alijinyakulia tuzo ya Mwandishi Bora wa Televisheni mwaka 2009, iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) alinaswa akipokea sh. milioni 10, kabla mtego aliowekewa haujafyatuka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajiwa kutoa taarifa za undani wa tukio hilo, Blog hii inafuatili kupasha kadri taarifa zitakavyopatikana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages