Breaking News

Your Ad Spot

Jan 22, 2010

MSHIKAJI ABAMBWA AKIJIFANYA SHOGA



IJANA mmoja wa Kiume wilayani Tarime mkoani Mara ametoa mpya baada ya kubambwa akijifanya shoga akiwa amevaa mavazi ya kike.

Kijana huyo kutoka Bukoba mkoani Kagera aliyetajwa kwa jina la Stephano Lucas (34) aka Anti Winfrida , amekamatwa na Polisi kanda Maalumu ya Tarime na Rorya akiwa Gesti ya Mowesiko mjini Tarime akiwa amevalia Kike huku akiwa na kifurushi cha bangi.

Mbele ya kamanda wa polisi kanda maalum ya tarime na Rorya, mshikaji huyo Stephano alikuwa hapo amevalia kike na kusuka nywele.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya , Costantine Massawe alisema kuwa Askari wake walipata taarifa ya kuonekana mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni mwanamme lakini amevalia nguo za Kike na anakunywa Pombe katika Bar ya Mowesiko huku akiwa amejitanda kwa ushungi.

Alisema baada ya kusmtukia polisi walimbamba mida ya saa 5 usiku na walipopekua chumba alichofikia Walikuta Kifurushi cha bangi.

Mdau-0788312145

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages