Breaking News

Your Ad Spot

Jan 26, 2010

RAIS SIRLEAF AGOMBEA TENA LIBERIA!!!!!!!


Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf  (Pichani) anasema ana nia ya kugombea kwa mara ya pili, licha ya kuahidi kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi tu kimoja cha miaka sita.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema anataka kumaliza dhana zinazotolewa juu ya nia yake ya kugombea mwaka 2011.
Msemaji wake Cyrus Badio amesema hakugundua kulikuwa na kazi kubwa ya kutekeleza kabla ya mwaka 2005, katika nchi inayojaribu kurejesha hali yake ya awali baada ya kuwepo kwenye vita kwa muda mrefu.
Sir Leaf ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais barani Afrika.
AAlishinda kwa 59% ya kura zote katika marudio ya uchaguzi dhidi ya mchezaji soka maarufu George Weah.

Source http://www.bbcswahili.com/

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages