Breaking News

Your Ad Spot

Jan 28, 2010

ZIARA YA DK. SHENI KENYA

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, akifukia mti alioupanda alipotembelea Taasisi ya utafiti wa madawa KEMRI mjini Nairibi jana. Makamu wa Rais yupo Nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu ya kiserikali.Mkuu wa shughuli za utafiti wa madawa katika taasisi ya utafiti wa madawa KEMRI Nchini Kenya Dk. Jimm Dennis, akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein kuhusu shuhuli mblimbali za utafti zinazofanywa wakati alipotembelea katika Taasisi hiyo jana. Makamu wa Rais yupo Nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu ya kiserikali.
Makamu wa Rais  Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka wakiangalia ng’ombe wa kisasa wa maziwa, wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Shamba la kilimo na mifugo la Dk. Musyoka katika kijiji cha Yatta Nairobi Kenya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia uandaaji wa huduma mbalimbali za mauwa wakati walipotembelea katika kiwanda cha mapambo mjini Nairobi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na watendaji wa kituo cha huduma za mawasiliano cha Safaricom, wakati walipotembelea kituo hicho Mlolongo Nairobi jana.
Picha zote na Mpigapicha wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Amour Nassor

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages