Breaking News

Your Ad Spot

Jan 29, 2010

KIBASILA SEC KWAWAKA MOTOLEO BAADA YA MMOJA KUGONGWA NA GARI

Mwanafunzi wa Kidato cha nne katika shule hiyo akisaidiwa na wenzake baada ya kupoteza fahamu wakati wa vurugu hizo.Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Mary Shayoi akisaidiwa na wenzake baada ya kupoteza fahamu baada ya kutokea vurugu zilizoitawanywa na po9lisi katika barabara ya Chang'ombe, karibu na shule hiyomjini Dar es salaam, baada ya mwanafunzi mmoja wa shule hiyokugongwa na gari.
Gari la huduma ya kwanza la hospitali ya Temeke likiwapeka hospitalini hapo wanafunzi walioumia na baadhi kupoteza fahamu katikatukio hilo.

Polisi wakifanya doria baada ya ghasia kutulia katika barabara ya Chang'ombe Dar es salaam. Ghasia hizo zilizofanywa na wanafuzni wa shule ya sekondari ya Kibasila baada ya mwenzao kugongwa na gari katika eneo hiloMgambo wakisaidiana kuondoa barabarani kizuizi kilichokuwa kimewekwa na wanafunzi katikati ya barabara ya Mandela, eneo la makutano ya barabara hiyo na Chang'ombe, wakati wa vurugu hizo jana.

STORY
ZAIDI ya Wanafunzi 20 wa shule ya sekondari, Kibasila,  Dar es Salaam, wameumia hadi baadhi ya kupoteza fahamu katika ya vurugu zilizotokea jana baada ya mwenzao kugongwa na gari katika barabara ya Chang'ombe.     Wanafunzi hao waliumia na baadhi yao kupoteza fahamu wakati Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) walipokabiliana na wanafunzi wa shule hiyo kuwataywanya baada ya kufunga barabara huku wakirusha mawe kwenye barabara ya Chang'ombe.
    Walioshuhudia walisema, vurugu hizo zilitokea saa 4 asubuhi, baada ya mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule hiyo Emmanuel Mapande kugongwa na gari katika barabara ya Chan'ombe, hatua chache kutoka makutano ya barabara hiyo na Mandela.
    Mwalimi wa shule, Agnes Charles wa shule hiyo, alisema, Mapande alipelekwa katika hospitali ya Temeke ambako alipatiwa matibabu na hali yake ilikuwa inaenmdelea vizuri.
    Alisema, baada ya mwenzao kugongwa wanafunzi walijawa na hasira na kufunga barabara kwa mawe huku wengine wakirusha mawe, hatua iliyofanya nagari kushindwa kupita eneo hilo kwa zaidi ya nusu saa.
     "Ndipo baadaye walikuja FFU na kupiga mabomu ya machozi na kusababisha wanafunzi kukimbia hovyo hadi wengine kuumia na wengine kupotza fahamu", alisema mwalimu huyo.
    Alisema, baadhi ya waliopoteza fahamu ni Agathha Kivunywa, Euster Hermitt, Fani Abdul, Kuruthum Athanas, Jacqueline Gades, Nary Richard, Janeth kagoa, Mary Shayo na Aneth Kiyogoma.
   Wanafunzi hao walipelekwa hospitali ya Temeke, kwa kuchukuliwa shuleni hapo na gari la wagonjwa la hospitali hiyo ambalo liliitwa kuokoa maisha ya wanafunzi hao.
   Wengine ambao walipekwa hospitali hawakuweza kufahamika mara moja kwa kuwa baadhi yao walaichukuliwas na walezi au wazazi wao waliofika shuleni hapo wakati wa vurugu.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke, Reberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo jana, kadhalika Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova hakulizungumzia.
   "Tukio hilo linahusu mkoa wa Temeke, mtafute Kamanda Sabas atakueleza kwa kina", alisema Kova alipopigiwa simu na mwandishi wetu.
    Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wanafunzi walitaka sasa eneo hilo lamakutano ya barabara ya Chang'ombe na Mandela lililopokaribu na shule hiyo liwekwe taa za kuongoza magari.
   Mwaka jana, ilipozuka tafrani eneo hilo baada ya amwanafunzi kugongwa, wanafunzi walidai yajengwe matuta hatua ambao ilitekelezwa, lakini licha ya kuwepo matuta ajali kamahiyo ya jana zimeendelea kutokea eneo hilo.

ciao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages