Breaking News

Your Ad Spot

Feb 17, 2010

VINYAGO VYA MPINGO VYATUMIKA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA!

KHALID Maunga (35) Mtanzania mwenye uraia wa Uingereza, akiwa chini ya ulinzi kwenye kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dakamatwa na dawa za kulevya, kete 69 aina ya Cocaine na kg 610 za bangi, juzi kwenye uwanja huo.
Kamanda wa Viwanja vya Ndege akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kukamatwa kijana huyo leo
Kamanda akionyesha kinyago cha faru kilivyochorongwa kujazwa dawa za kulevya.

STORI
KIJANA mmoja mzaliwa wa Tanzania, raas wa Uingereza, amedakwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akidaiwa kutaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine na Bangi ambavyo inadaiwa alivificha katika vinyago na pindo za suruali.
Akizungumza  ofisini kwake, leo Kamanda wa kikosi hicho Mwajuma Kiponza, alisema Maunga alikamatwa baada ya kukaguliwa katika mashine ya kawaida wakati akiingia uwanjani na akafanikiwa kupita.
  Alisema baadaye polisi walimtiliashaka na kuamua kumkagua zaidi maungoni na kumkuta akiwa na  pipi 69 za dawa za kulevya aina ya Cocaine na gramu 610 za bangi.
     Kamanda Mwajuma alisema Maunga (35) alikamatwa jana saa 1.30 asubuhi kwenye uwanja huo, akiwa tayari kwa safari ya kwenda Ungireza, kwa Ndege ya  Shirika la ndege la Uingereza akiwa na paspoti namba 10948353, iliyotolewa mwaka 2007 nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages