Breaking News

Your Ad Spot

Feb 9, 2010

MECHI YA LIGI KUU YA VODA TANZANIA BARA, SIMBA YAIUA MANYEMA FC 2-0

                                                             HABARI KATIKA PICHA
MCHEZAJI wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi' akipambana na Shaabani Ramadhani (kulia) kuwania mpira, timu hizo zilipomenyana jana, kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania Bara. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
MCHEZAJI Stanley Minzi wa Manyema FC (kushoto) akianguka na Ramadhani Chomo wa Simba katika harakati za kuwania mpira, timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, katika Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania Bara. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
WACHEZAJI wa simba wakishangilia baada ya kupata abao la kwanza katika kipindi cha pili dhidi ya timu ya Manyema FC, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
BENCHI la ufundi la timu ya Manyema FC wakiwa wameduwaa baada ya mechi kumalizika timu yao ikiwa imefungwa mabao 2-0 na Simba katika mecho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana. Katikati ni Kocha Mkuu wa timu hiyo Abdallah Kibadeni King na Makocha wasaidizi Shekhe Abdallah na Yasin Napili.
WACHEZAJI wa Manyema FC wakimzonga refa baada ya kuipatia Simba penati iliyozaa bao la pili.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages