Breaking News

Your Ad Spot

Feb 5, 2010

TASAF YATINGA UMOJA UN

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Dk. Servacius Likwalile (shoto)akisisitiza jambo wakati wa mjadala kuhusu uhusiano kati ya ushirikishwaji wa Jamii , utokomezaji wa umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi, mjadala huo umefanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York leo. Anayemsikiliza kwa makini ni Waziri wa Masuala ya Jamii na Ajira wa Netherlands, Donner wengine katika picha ni jopo la walioshiriki mjadala huo. (Picha na habari kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa)


       "Ushirikishwaji wa wananchi maskini kupata ajira ni muhimu"
Juhudi za nchi zinazoendelea za kuutokomeza umaskini na upatikaji wa ajira zenye hadhi na tija, hazitaweza kufanikiwa kama wananchi maskini na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi, hawatashirikishwa katika utoaji na upitishaji wa maamuzi yanayohusu mustakabali wao.
    Ushauri huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Dk. Servacius Likwelile, wakati wa majadiliano kuhusu dhana ya uhusiano kati ya ushirikiwaji wa jamii, utokomezaji wa umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi.
    Majadiliano hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Maendeleo ya Jamii.
     Dk.Likwelile ambaye alikuwa mmoja wa wanajopo wanne walioshiriki majadiliano hayo, amewaeleza wajumbe waliokuwa wakifuatilia majadiliano hayo kwamba, kunauhusiano au muuingiliano mkubwa kati ya ushirikishwani wa wananchi na utokomezaji wa umaskini na upatijanaji wa ajira.
    Maafanikio yoyote katika upunguzaji wa umaskini, unategemea sana pamoja na mambo mengine upatikanaji wa fursa kwa watu maskini kupigania haki zao kwa kupitia mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoja na taratibu za kisheria. Inataka ushirikishwaji madhubuti wa jamii hiyo katika shughuli za uendeshaji wa uchumi na hasa zile zenye manufaa kwao”. akabainisha Dkt. Likwalile.
   Akaeleza kuwa licha ya juhudi mbalimbali za kitaifa na kimataifa za kuanzisha mipango na sera za kuutokomeza umaskini, takwimu zinaonyesha idadi ya watu wanaoishi katika umaskini imeongezeka kutoka 190 milioni mwaka 1990 hadi milioni 380 mwaka 2005.
    Wengine walioshiriki mjadala huo ni Dkt. Beatriz Merino kutoka Peru, Bw. J. Piet Hein Donner Waziri wa Wizara ya Masuala ya Jamii na Ajira kutoka Netherlands na Profesa Vojtech Tkae ambaye ni mshauri wa Waziri wa Ajira , Masuala ya Jamii na Familia nchini Slovakia.
    Kama hiyo haitoshi Dkt Likwelile anaongeza kuwa unyimwaji wa haki za jamii ni mkubwa, kutengwa kwa watu maskini ni jambo la kawaida na ukosefu wa huduma za msingi za jamii ni jambo la kawaida katika nchi nyingi hasa barani Afrika.
   Akasema ni muhimu pia kwamba haki za kijamii na za kisiasa zikajielekeza zaidi katika uwezeshwaji wa watu maskini na sit u katika kudai haki zao za kiuchumi na kijamii lakini pia kudai uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma bora za jamii, sera zinazowajali wanyonge na uwazi katika mchakato mzima wa ushiriki wao.
     Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TASAF akaeleza kuwa ,Tanzania kupitia mfuko huo imejitahidi sana kuwashirikisha wananchi maskini na wanaoishi katika mazingira magumu, kushiriki na kupitisha maamuzi ya miradi inayolenga kuwaondolea umasikini na kuwapatia ajira.
     Alitoa mfano kwa kusema,TASAF huwapa fursa wananchi katika ngazi ya kijiji au eneo wanaloishi kuchagua ni aina gani ya mradi wa maendeleo wanaoutaka, ushiriki wao katika utekelezaji wa mradi huo, udhibiti na matumizi ya fedha za mradi huo pamoja na kuangalia ni familia gani iliyokatika mazingira magumu inayostahili kupata ajira kupitia mradi huo.
    “Tanzania kama zilivyo nchi nyingi za Afrika, asilimia 34 ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa upatikanaji wa huduma za msingi, huku asilimia 18 wakiwa katika umaskini wa upatikanaji wa chakula. Kwa hiyo mifuko ya jamii kama tasaf na mingineyo pamoja na mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini ( Mkukuta) malengo yake ni kutoa fursa za ushirikishwaji wa jamii” akasema.
    Kuhusu mweleko wa baadaye katika dhana hiyo ya ushirikishwaji wa jamii na uhusiano wake katika kuutokomeza umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi, Dkt likwalile anasema juhudi za makusudi pamoja na utashi wa kisiasa kutoka kwa makundi mabalimbali ya viongozi wa kisiasa, taasisi za kijamii, washiriki wa maendeleo zinatakiwa katika kuhakikisha kuwa mwananchi maskini anashiri katika mambo yanayomhusu.

1 comment:

  1. Naked Celebrities Exposed. [url=http://duringarticles.info/celebrity-stolen-clips.html]duringarticles.info[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages