Breaking News

Your Ad Spot

Mar 11, 2010

BREAKING NEWS!!!!!

Daktari Mwandamizi afariki Dar kifo cha kutatanisha

DAKTARI Mwandamizi wa Hospitali ya St. Bernard ya mjini Dar es Salaam, Dk. Elias Mrutu (50) amnefariki dunia, usiku wa kuamkia leo, mazingira ya kifo chake  yakidaiwa kuwa ya kutatanisha, yakihusishwa na mzozo wa kifamilia.
   Kwa mujibu wa Dk. Linus Chuwa, ambaye ni Mkurugenzi  Mkuu wa hospitali hiyo, juzi saa tisa alasiri Dk.Mrutu alitoka kazini (St. Bernard), akiwa hana tatizo lakiafya.
   Alieleza kuwa Dk. Mrutu akiwa nyumbani kwake Magomeni baada ya kula chakula saa 4 usiku alianza kutapika damu mfululizo.
   Dk. Chuwa alidai, kwa mujibu wa taarifa alizopata, watoto wake na majirani walipotaka kumpeleka hospitali alikataa, na saa 10 usiku wa kuamkia leo, alipata simu ya kuomba gari kwa ajili ya Dk.Mrutu kupelekwa hospitali.
   Alisema saa 12, asibuhi mmoja wa watoto na watiu wengine watatu walimfikisha St. Bernard na alishangaa kuona mwili wa Dk. Mrutu umetapakaa damu.
   Alisema katika uchunguzi aligundua kwa Dk. Mrutu amekwishafariki dunia tangu nyumbani au njiani alipokuwa akiletwa.
   mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages