Breaking News

Your Ad Spot

Mar 3, 2010

CAPELLO ALAUMU MALIPO YA WACHEZAJI

Meneja wa Uingereza Fabio Capello (Pichani), amelaumu pesa nyingi wanazopewa wachezaji wake kwa mizozo inayowakumba.

    Capello anasema mizozo hiyo, ambayo inatishia kuathiri matumaini ya timu ya Uingereza katika kombe la dunia, imekumba wachezaji katika nchi zingine pia kama vile Italia, Ujerumani na Uhispania.
    Wachezaji kadhaa wa timu ya Uingereza wamehusika katika mizozo ya kimapenzi hivi majuzi. Kapteni wa timu hiyo John Terry alitimuliwa kutoka wadhfa wake kufuatia mzozo wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa mchezaji mwenzake katika timu ya Chelsea hapo zamani, Wayne Bridge.
   Bridge, ambaye hakumsalimia Terry wakati timu anayoichezea, Manchester City ilikutana na Chelsea wikendi iliyopita, amesema kwamba hataichezea timu ya Uingereza kwa sababu ya mzozo huo.
    Mchezaji mwingine wa timu hiyo, Ashley Cole, pia aligonga vichwa vya habari mwezi jana baada ya kuachana na mke wake Cheryl. Timu hiyo ya Uingereza itakutana na Misri hii leo. http://www.bbcswahili.com/

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages