Breaking News

Your Ad Spot

Mar 25, 2010

KILIMANJARO PREMIUM KWA KUSHIRIKIANA NA BASATA WATANGAZA NYIMBO NA WASANII WATAKAOCHUANA TUNZO YA MUZIKI TANZANIA

KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium kwa kushirikiana na Barza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza wateule kumi walioingia katika mpambano wa tuzo za muziki Tanzania ambao utaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu.
    Akizungumza leo makao makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tuzo hizo, Angelo Luhala kutoka Basata, amesema ushindani utakuwa katika kupata maimbaji Bora ambapo waliopatikana kuchuana katika fungu hilo ni Lady Jaydee, Mwasiti, Maunda Zoro, Vumilia na Khadija Yussuf .
    Kundi la pili ni Mwimbaji bora wa kiume Marlow, Banana Zorro, Mzee Yussuf, Ali Kiba na Chiristian Bella,
   Alisema kundi la tatu ni Albamu bora ya taarab ambazo ni  Daktari wa Mapenzi (Jahazi Modern Taarab), Riziki Mwanzo wa Chuki (5 Stars Modern Taarab), Kukupenda isiwe taabu (Coast Modern Taarab), Powa Mpenzi (New Zanzibar Star na kila mtu kivyake vyake ya East African Melody.
   Upande wa wimbo bora wa taarab, zitachuanishwa nyimbo za Daktari wa mapenzi (jahazi Modern Taarab), Wapambe Msitujadili (5 Stars Modern Taarab), Riziki mwanzo wa Chuki (Khadija Yussuf), Roho mbaya haijengi (Jahazi Modern Taarab ) na Kukupenda isiwe taabu (Coast Modern Taarab).
     Kwa upande wa Wimbo bora wa mwaka  ni Pii Pii-Missing my baby ( Marlow), Kamwambie (Diamond), Zoba (Banana Zorro),  Nikipata nauli (Mrisho Mpoto) na Kwa ajili yako (Hussein Machozi).
    Alisema kinyang'anyiro cha Bendi yenye wimbo bora wa Kiswahili (bendi) ni Nilizama (Machozi band), Mwana-Dar es Salaam (African Stars), Asha (Top Band), Vuta nikuvute (FM Academia) na Mjini Mipango wa Extra Bongo,  huku katika albamu bora ya bendi zikiumanishwa Mwana-Dar es Salaam (Aftrican Stars), Hilda (Diamond Muzica) na huna shukurani wa Masondo band.
    Katika wimbo bora wa asili ya Kitanzania ni Nikipata nauli (Mrisho Mpoto), Mtarimbo( Machozi  band), Samaki (Offside Trick),  Chei chei ( Wahapa Hapa band) na kupata majaaliwa wa Omari Omari.
    Nazo nyimbo bora za R&B zitakazochuana kuwania tuzo ni  Masogage (Belle 9), Kamwambie (Diamond),  Nipigie (Stara Thomas),Mapenzi ya wawili (Maunda Zorr) na sogea karibu wa Steve na kwa upande wa  wimbo bora wa Hip Hop ni  Stimu zimelipiwa(John Makini), Bullet (Quick Racka), Pom Pom Pisha (Chid Benz), CNN (Mangwea)  na Im Professional wa Fid Q.
     Zile za Reggae zitakazochuana kupata mmoja ulio bora ni Alcohol (Hemed),  dont let i go (Dabo na Mwasili), Barua (Man Snepa), Umoja ni Nguvu wa Matonya na Christian Bella na Leo (reggae Remix) wa AY.
Upande wa nyimbo za Ragga ni Shikide (Dully Sykes), Mungu yuko bize (Bwana Misosi), Wasanii 9Drezzy Chief) na fly wa Benjamini wa mambo jambo, huku mpambano wa rapa bora wa mwaka ukiwakutanisha  Khalid Chokoraa, Ferguson, Kitokololo, Totoo Ze Bingwa na Diof.
   Alisema, upande wa msanii bora wa Hip Hop watanyukana John makini, Fid Q, Chid Benz, Magwea na Profesa Jay huku watunzi bora wanaochuana kupata aliye bora wakiwa ni  Mzee Yussuf, Mrisho Mpoto, Lady jay Dee, banan Zorro, Mzee Abuu na Fid Q.
   Upande wa wimbo bora wa afrika Mashariki  ni Where you are ( Blue 3 na radio and Weasal (Goodlife), Haturudi nyuma (Kidumu na Juliana), Na wewe (Cindy), Bread and Butter (Radio and Weasal- Googlife) na umenikosea wa Kidumu.
    Upande wa mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka ni Marcol Chali, Hermy B. Allan Mapigo na Man Water huku upande wa video bora ya mwaka zikipambanishwa  Natamani kuwa malaika (Lady Jay Dee), Kamwambie ( Diamond), Leo( A.Y), Zoba (banana Zorro),  problem (C Pwaa).
    Alitaja nyimbo za afro Pop zitakazochuana kuwa ni  Zoba (Banana Zorro), Msiniseme (Alikiba), Pii Pii (Marlow), Mama mubaya (Mataluma na Karibu kiumeni wa Chege. huku wasanii bora wanaochipukia watakaochuana kumpata mwenzao bora kuwa ni  Belle9, Diamond, barnaba, quick Racka na Amini.
   Alisema, kwa upande wa wimbo bora wa kushirikiana kimbembe kitakuwa baina ya nyimbo za Nipigie (At-Stara Thomas), CNN ((Mangwea na Fid Q),  Njia panda (Barnabas, Prof Jay na Sugu) na utaipenda wa Hussein Machozi na John Makini
    Luhala alisema uteuzi wa nyimbo au wasanii wanaoingia kwenye kinyang'anyiro hiocho wamepatikana baada ya mchakato uliosimamia na Deloitte Consulting Company ambapo wadau 100 walikaribishwa kuwakilisha Tanzania kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga, Mbeya na Zanzibar.
      Alisema, kampuni hiyo ya Deloitte itaendelea kuwa msimamizi wa kuhakiki na kuhesdabu kura za wadau na kubaki na matokeo hadi utoaji wa tuzo utakapofanyika May 14, mwaka huu.
Ofisa Mshauri wa kampuni ya Delloitte, Neema Mwengu akikabidhi bahasha zenye uteuzi wa wasanii au nyimbo zitakazozishiriki katika kinyang'anyiro cha Tuzo la Muziki Tanzania (Kilimanjaro Muzic Award) kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja, leo katika ofisi za TBL mjini Dar es Salaam. Katikati ni Mtaribu wa shindano hilo Angelo Luhala kutoka Baraza la Muziki Tanzania (BASATA) ambaye baadaye alikabidhiwa na Minja kutangaza uteuzi huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages