Breaking News

Your Ad Spot

Mar 25, 2010

WATU KUMI WAMEKUFA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA DALADALA KUANGUKIWA NA LORI KIBAMBA LEO

HIVI ndivyo hice lilivyoangukiwa na kupondwa vibaya na lori lenye tanki la mafuta, na kusababisha vifo vya watu kumi leo!!!!!
STORI
WATU wamekufa papo hapo leo saa 10.30 alfajiri, baada ya lori lenye namba T 189 ABP na tela la mafuta lenye namba T 192 ABP  lililokuwa likitokea  Dar es Salaam kwenda mkoa wa Pwani kupinduka hadi kuliangukia basi dogo la abiria la ina yaToyota Hiace lenye namba T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,
     Basi hilo dogo la Hiace ambalo limepondwa vibaya  likiwa na abiria ndani lilijkuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na watu kumi ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.
      Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.
     Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.
      Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali. Taarifa zaidi kuhusiana na ajali hizo zitaendelea kutolewa kadri zitakavyopatikana

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages