Stori kwa Ufupi
MAHAKAMA ya hakim Mkazi mkoa wa Arusha imemuona Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka hana hatia katika mashitaka yaliyokuwa yanamkabili ya kutihsia kuua kwa bastola na kudhuru mwili.
Katika hukumu yake hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Devotha Msoffe alitoa uamuzi huo baada ya kupitia mwenendo mzima wa kesi iliyokuwa ikisikilizwa na hakim James Kaalyamaha aliyehamishwa kazi kutoka amahakama hiyo.
Alisema hakuna shitaka linalomtia hatiani mbunge huyo na kwamba kesi hiyo ilikuwa ya kutengenezwa kutokana na kwamba ushahidi uliotolewa ulikuwa ukijikanganya katika maeneo mengi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269