Breaking News

Your Ad Spot

Mar 5, 2010

MKUTANO WA WANAWAKE NEW YORK: WANAWAKE WANA UWEZO WA KUONGOZA NCHI-MONGELA

Mbunge wa Peramiho na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Jenista Mhagama akifuatilia mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Hali ya Wanawake, kulia kwake ni Mkurugenzi wa jinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bw Mechack Meliyo NdaskoiWajumbe wa kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishiriki mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu hali ya wanawake. Mstari wa Mbele kushoto ni Bi Rahma Khamisi,Mkurugenzi Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto. Katibu Mkuu Bi Rahma Mshangama, wengine ni Mwanaidi Salehe Abdalla, Bi. Mariam Mwafisi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi Wahida Mohammed, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Wanawake.
STORI 
Na Mwandishi Maalum, New York
 Imeelezwa kwamba, mwanamke wa Afrika anauwezo kwa kushika madaraka makubwa ya kiserikali yakiwemo ya kuongoza nchini.
    Maelezo hayo yametolwa na Dkt. Getrude Mongela, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa wanawake uliofanyika Jijini Beijing China mwaka 1995.
    Ametoka kauli hiyo wakati akichangia mjadala kuhusu miaka Kumi na Tano ya Tamko la Beijing –‘ajenda ambayo haijakamilika’.
    Akamtaja Rais wa Liberia, Ellen Johson- Sirleaf ambayeni mwanamke wa kwanza barani Afrika kuwa kiongozi mkuu wan chi kwamba ni ni mfano hali wa kwamba wanawake wanaweza.
    “ Ninachoweza kutaja kama changamoto, miaka kumi na tano baada ya Tamko la Beijing ni kwamba , wanawake bado hawajashika madaraka makubwa ya kiserikali , serikali nyingi bado zinashikiwana kuendeshwa na wanaume ukiondoa ile ya Liberia. Hili ni tatizo kwa sababu wanaume bado ndio watoa maamuzi wakubwa katika taasisi mbalimbali za kiserikali”. Anasema Dkt. Mongela
    Na Kuongeza .“Kabla ya Tamko la Beijing, nani aligetemea kama mimi ningeweza kuwa Spika wa kwanza mwanamke wa Bunge la Umoja wa Afrika. Miaka kumi na tano iliyopita hapa kuwa na Rais Mwanamke katika ardhi ya Afrika lakini leo tunaye Ellen Johnson- Sirleaf ambaye alisimama kidete kwaajili ya Liberia:”.
   Dk. Mongela ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ukerewe, alishangiliwa sana na wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake ,wakati alipotambulishwa kama mmoja wa washiriki wa majadiliano hayo.
   Mongela ambaye alikuwa mmoja wa wanajopo katika mjadala huyo, ambao ulifanyika mara baada ya Katibu Mkuu Ban Ki Moon kusoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwanamke ambayo imefanyika March Moja hapa Umoja wa mataifa.
   Akielezea ni jambo gani linalomfanya mwanamke wa Afrika awe tofauti na wengine. Mongela anasema jambo kubwa linalomtofautisha mwanamke wa afrika ni utu na hadhi yake.
   ”tofauti kubwa ya mwanamke wa kiafrika ni utu na hadhi aliyonayo, mwanamke wa kiafrika daima husimama kidete na ni mpiganaji. Na tamko la Beijing la mwaka 1995 limewapa fursa na nafasi nzuri ya kupigania na kutafuta haki zao” anabainisha.
   Na kuongeza kwamba jumuia ya kimataifa inatakiwa kulitambua . na pia kujifunza kwmaba Tamko la Beijing limempa mwanamke nguvu ya kupiga hodi na kufungua milango ya majadiliano.
   Alisemani tamko ambalo limemuweka mwanamke karibu zaidi na mwanaume na mwanaume kuwa karibu zaidi na mwanamke.
   “ Leo hii kila mtu anatambua kwamba mwanamke naye anayohaki ya kuishi katika dunia. Wanatambua kuwa mwanamke na mwanaume lazima washirikiane. Kwa sababu hata wanawake walishiriki katika kupingania uhuru wan chi zao. Wanaume hawana namna nyingine zaidi ya kukubali” anasisitiza Mongela.”
   Alitoa mwito kwa wanawake kutoka kata tamaa kwani hatua kuna mafanikio ambayo yamekwisha kupatikana baada ya tamko la Beijing. Na kinachotakiwa ni kuongeza kasi ya kutekeleza yale ambayo bado yajafanyiwa kazi.
   Pia aliwahamasisha wanawake kujihusisha na kushiriki kikamilifu kuyatafutia ufumbuzi matatizo yatokanayo katika nchi zao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages