Breaking News

Your Ad Spot

Mar 6, 2010

SIKU CHACHE BAADA YA KUUAWA WATU 17 WA UKOO MMOJA, WENGINE WATANO WAMEUWA HARUSINI TARIME

WATU watano wa ukoo mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi na kukatwa mapaanga wakiwa harusini katika kijiji cha Kimusi, Kata ya Nyamwaga, tarime mkoani Mara.
   Mauaji hayo yametokea ikiwa ni siku chache tangu watu 17 pia wa ukoo mmoja kuuawa usiku katika mtaa wa Bugharanjabho kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma mkoani humo.
   waliouawa katika harusi juzi, ni wa ukoo wa Wairegi na wametajwa kuwa ni Mwita Mathias, Matoka sokoni,  Chacha Munyoro,  Wangwe Wambura na Magaiwa Makene, inadaiwa wameuawa na watu wa ukoo wa  Nyabansi.
     Taarifa zimesema waliouawa walikuwa katika harusi nyumbani kwa Mwita Gurugu  mkazi wa Kimusi na kwamba mbali na mauaji hayo watu saba wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya  Tarime.
    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Rorya na Tarime Costantine Massawe alisema mauaji hayo inaelekea ni ya kulipiza kisasi.
  Alisema kabla ya tukio hilo,  mtu aliyemtaja kwa jina la Samson aliporwa ng'ombe 30, waliodaiwa kuingizwa katika kijiji cha Kimusi na baadaye kupelekwa kijiji cha Kegonga nchini Kenya.
    

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages