Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2010

KILI TAIFA CUP KITO CHA IRINGA, IRINGA YANG'AA KWA BAO LA PENATI

NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
PENATI pekee amabayo timu ya Ruaha Stars ya Iringa iliipata katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza jana iliiwezesha timu hiyo kuibuka kidedea dhidi ya Ruaha Stars ya Mbeya, katika mechi ya mzunguko ya Kili Taifa Cup, iliyopigwa baina ya timu hizo katika uwanja wa Samora mjini hapa.

Penati hiyo ambayo ilipigwa na mshambiliaji wa timu hiyo, Athumani Iddy ‘Chuji’ ilipatikana baada ya mchezaji wa Mbeya Baraka Haule kucheza rafu ndani ya eneo la hatari la timu yake.

Licha ya Mbeya kufugwa bao hilo na kulalaa nalo hadi kipindi cha mwisho matokeo yakiwa bao 1-0, timu hiyo ilionyeshana nguvu sawa na Iringa ambao ni wenyeji katika kituo E cha mjini hapa.

Tangu mwanzo wamchezo timu zote zilionyesha kuwa na ari ya kutakakuibuka ana ushindi, lakini ukiacha penati ambayo Iringa ilipata, mashyabulizi ya kila timu dhindi ya mwenzake hayakuweza kuzaa matunda katika umaliziaji.

Kwa upande wa Iringa mashambulizi yake mengi yaliambana na kona ambazo ilizipata nne,mbili kipindi cha kwanza na nyingine cha mwisho huku Mbeya wakipata kona mbili katika kipindi cha mwisho.

Hadi kipindi cha mwisho Mbeya haikufanaya mabadiliko kwa wachezajai wake, lakini Iringa katika dakika ya 58 kipindi cha pili, ilimtoa George Haule na kumwingiza ussa Mgunda zikiwa ni harakati zakocha wa timu hiyo Freddy Felix Minziro kutaka kupata mabao zaidi.

Kufuatia matokeo hayo, sasa Iringa imeshinda amechi moja na kutoka sare mechi moja ambayo ilicheza na Kinondoni, huku Mbeya nayo ikiwa imepoteza mchezo wa jana mmoja na kuifunga bao moja timu ya Rukwa.

Mbeya: Abdulrazak Jackson, Mashaka David, Baraka HauleDavid Mwandika,Juluus Mwalukasa,Msafiri Hassan,Mwagane Yeya,Patson Chawinga, Gaudence Mwaikimba,Benjamin Msokile na Daniel,Mashaka.

Iringa: Odo Nombo, Charles Abwene,Lugano Mwagamabeta,Lwitiko Mwakalasa, salum Swed Godfrey Bonny,Brighton Mponzi, Athumani Iddy 'Chuji', JumaKhalifa na George Haule/Mussa Mgunda.

Kesho ni mapumziko hadi keshokutwa ambapo keshokutwa zitashuka dimbani Rukwa na Iringa mechi ya mchana na Kinondoni na Mbeya Mechi ya jioni.

Katika michuano hiyo ambayo robo fainali hadi fainali zitafanyika mjini Dar es Salaam,katikauwanja wa Uhuru, wadhamini wake Kampuni ya BIta Tanzania TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Prenier Lager, wametenga mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuyanogesha ambapo mshindi wa kwanza atakapaa sh. milioni 35, wa pili sh. milioni 20 na watatu akipata sh. milioni tano.

TBL haikuishia hapo tu upande wa zawadi kwa kuwa mchezaji bora,Kipa bora,mwamuzi bora,mfungaji bora, kocha bora na timu yenye nidhamu watapata kibundfa cha sh. milioni mbili kilammoja.

mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages