Breaking News

Your Ad Spot

May 11, 2010

BAADA YA KUIKANDIKA PINDA BOYS 4-0 JANA, KESHO KINONDONI INASHUKA DIMBANI NA MBEYA

BAADA ya kuikandika jana mabao 4-0 timu ya Rukwa 'Pinda Boys'  timu ya Kinondoni inashuka dimbani na Mbeya katika mechi ya mwisho ya  mzunguko wa michuano ya Kili Taifa Cup itakayopigwa Uwanja wa Samora mjini hapa.

Kinondoni iliichapa jana timu ya Rukwa katika mechi iliyoanza saa 10 jioni, ikiifuatia ile ya Iringa na Mbeya iliyoanza saa 8 mchana na kumalizika huku Iringa ikiwa imeibuka na ushindi wa bao 1-0, bao ililolipata kwa penati.

Mechi ya Kinondoni na Mbeya itatanguliwa na mechi baina ya timu ya Rukwa na Iringa ambayo itaanza saa 8 mchana.

Kulingana na matokeo yaliyokwisha patikana katika mechi zilizotangulia za makundi, katika kituo E cha Iringa, Kinondoni na Iringa ndizo zenye mtaji mzuri wa mojawapo kuweza kuongoza katika kundi hilo na hivyo kuweza kufunzu kucheza robo fainali mjini Dar es Salaam.

Hadi sasa Kinondoni ina jumla ya pointi nne ikiwa imefunga mabao matano ya kufungwa na moja la kufungwa, huku Iringa ikiwa na poiti kama hizo lakini mabao pungufu ambayo ni mawili ya kufunga na moja na kufungwa.

Timu ya Rukwa ndiyo inaongoza kwa kufungwa mabao mengi ambapo hadi sasa imefungwa mabao matano huku yenyewe ikiwa haina bao nayo Mbeya ikiwa imefungwa mabao mawili na kufunga moja ililolipata katika mechi yake dhidi ya Rukwa mwanzoni mwa michuano hiyo.

Katika michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, mshindi wa kwanza atajizolea sh. milioni 35, wapili sh. milioni 2 na watatu sh. milioni tano, huku mchezaji bora,kipa bora, mwamuzi bora, mfungaji bora na timu yenye nidhamu wakipata sh. milioni mbili kila mmoja.

Katika kituo cha Iringa michuano hiyo itamalizika ikiwa imeonyesha msisimko mkubwa kutokana  kuhudhuriwa na mashabiki wengi katika mechi hasa za nyakati za jioni.

Pia itaacha historia nzuri kutokana na wachezaji chipukizi kuweza kuonyesha vipaji vya hali ya juu kwa kuwakabili vilivyo baadhi ya wachezaji waliokwishachezea Ligi Kuu na hadi katika timu ambazo zimewahi kutwa ubingwa wa Ligi hiyo kama Simba na Yanga.

Iringa ndiyo imeonyesha kuwa na wachezaji wengi zaidi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara kama kina,  Athumani Iddi 'Chuji' na Godfrey Bon wa Yanga, Kipa Odo Nombo wa Manyema Rangers,  Salum Swedi wa Mtibwa Sugar na Yona Ndabila kutoka Moro United.
========================================
PICHA KINO NA PINDA BOYZ

BEKI wa timu ya Rukwa 'Pinda Boys' Aplai Kong'oa (kulia) akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Kinondoni, Shaibu Nayopa, timu hizo zilipomenyana juzi katika Uwanja wa Samora, mjini Iringa, katika mechi ya mzunguko ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup'. Pinda Boys ilibnyukwa mabao 4-0.
 RASHID Rosha wa timu ya Kinondoni (kushoto0 akipambana na mchezaji wa Rukwa 'Pinda Boys', Ahmad Yahya, timu hizo zilipomenyana juzi katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika mechi ya mzunguko ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup'. Pinda Boys ilibnyukwa mabao 4-0. (Picha zote naBashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages