Breaking News

Your Ad Spot

Jul 23, 2010

MTAALAM WA KODI AMINA MKUMBA AOMBA KUWANIA UBUNGE KIBITI, RUFIJI MKOA WA PWANI: AKIPITA ATAKUWA MWANAMKE WA KWANZA KUTOKA ENEO HILO KUWA MBUNGE, BAADA YA BIBI TITI MOHAMMED

MSOMI wa masuala ya Usimamizi wa kodi, Kada wa CCM Amina Mussa Mkumba (29) akirejesha fomu yake ya kuwania Ubunge jimbo la Kibiti, wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, jumatano wiki hii, kwa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Joseph Pandisha. Amina ambaye ni msomi mwenye Stashahada ya Uzamili ya usimamizi wa Kodi, akichaguliwa atakuwa mwanamke wa pili kuwa mbunge katika wilaya hiyo, baada ya aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri nchini, marehemu Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza.


STORI

MSOMI wa masuala ya usimamizi wa kodi  Amina Mussa Mkumba (29), amejitosa kuwania ubunge jimbo la Kibiti, wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani,  kwa tiketi ya CCM.

Akizungumza na baada ya kurejesha fomu yake ya maombi kwa Katibu wa CCM Wilaya  hiyo, Joseph Pandisha, alisema, ameigia katika kinyang'anyiro hicho kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuweka rekodi ya kuwa mwanmke wa pili kuwa mbunge wa jimbo hilo, baada ya aliyekuwa mkongwe wa siasa nchini, Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza katika wilaya hiyo.

Msomi huyo mwenye stashahada ya juu (Advanced Diploma) na Stashahada ya Uzamili,(Post graduate Diploma) alizopata katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam, alisema, pia lengo lake ni kuitika mwito wa Rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa kuwataka wanawake nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

"Kimsingi nina malengo mengi, lakini baadhi yake ni la kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa pili kushina Ubunge hapa U-ndengerekoni, baada ya Mama yetu, Bibi Titi Mohammed aliyekuwa wa kwanza ambapo baada ya yeye hajatokea tena mwananamke mwingine kushika ubunge", alisema na kuongeza, "tena nafanya hivi kwa kuwa naunga mkono mwito wa Rais wetu, na Chama Cha Mapinduzi kwamba wanawake tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi'.


Amina alisema mwanamke anayeacha kujitokeza kuwania uongozi wakati anaona ana uwezo wa kufanya hizo, ni kama anapuuza mwito wa Rais Kikwete na Chama Cha Mapinduzi, jambo ambalo si sahihi.

Mbali na Amina, pia wamejitokeza wana-CCM kadhaa kuwania ubunge wa jimbo hilo akiwemo mbunge za zamani aliyemaliza muda wake, Abdul Marombwa anayetetea kurejea tena.

Chachandudaily Blog  inamtakia kila la kheri katika kusaka nafasi hiyo

1 comment:

  1. Hongera sana dada Amina kwa kujitokeza Kuwania ubunge jimbo la kibiti.wanawake pia mnaweza jitahidi utashinda. Nakutakia kila la kheri katika kinyang'anyiro hicho

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages