Breaking News

Your Ad Spot

Aug 19, 2010

WAGOMBEA SITA WA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM WAKOSA UPINZANI MAJIMBONI MWAO

WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi imehitikisha leo muda wa urudishaji fomu za kuwania urais na ubunge kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu, zimepatikana taarifa kwamba hadi saa 10 jioni, ambao ni saa ya mwisho, wagombea wa sita wa CCM walikowa hawakupita upinzani katika majimbo yao.

Taarifa hizo za uhakika zimethibitisha kwamba, wagombea hao mbao kulingana na hali hiyo watangazwa na NEC kuwa wamepita bila kupigwa ni pamoja na  Januari Makamba (Bumbuli).

Wengine na majimbo yao yakiwa katika mabano ni, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (Isimani), aliyekuwa Naibu Spika, Anna Makinda (Njombe), Job Ndugai ( Kongwa), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Gregory Teu katika jimbo la Mpwapwa.

Kutoakana na umuhimu wa taarifa hii, blogu yako ya Jamii, Chachandu Daily, inaendelea kukuhanbarisha yatakayojiri zaidi

1 comment:

  1. Shukran sana anko Bashir kwa 'chachandu daily' ninakusoma na leo ni mara yangu ya kwanza kukufahamu na kufika hapa, tayari nimevutiwa sana na habari unazoandika. Shukrani sana Bashir!

    Mimi Subi wa wavuti.com

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages