Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii, Teddy Mapunda kutoka kampuni ya bia ya Serengeti akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana ndani ya hoteli ya Movernpick,jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa shindano la Tusker Project Fame kwa awamu ya nne,Teddy amefafanua kuwa nia na madhumuni ya kufanya shindano hili hapa Tanzania ni kutaka kuinua vipaji vya Watanzania hapa Tanzania.
Tusker Project Fame kwa mwaka huu itakuwa inashirikisha nchini nne ikiwemo. Kenya,Uganda,Rwanda,Tanzania pamoja na Sudani ya Kusini.Aidha Teddy amesema kuwa usahili kwa ajili ya shindano hilo utafanyika katika hoteli ya Peacock-Mnazi Mmoja siku ya jumamosi kuanzia saa 2 asubuhu mpaka saa 11 jioni.Amesema kuwa washiriki wa shindano hilo ni lazima wawe na umri wa miaka 23 na kuendelea na wawe na vitambulisho vyao kuhakiki umri wao,"fomu za kujiunga zinapatikana Mlimani City, Benjamin William Mkapa Towers, IPS Building pamoja na sehemu ya usahili wenyenyewe pale Peacock Hotel",amesema.
Meneja Matukio, Bahati Sigh akifafanua zaidi kuhusu mchakato mzima wa ushiriki wa shidano la Tusker Project Fame,ambalo limezindua kampeni yake ya nne katika hoteli ya Movernpick, leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, Mawasiliano na Jamii, Teddy Mapunda na kulia nii Mshauri wa Masoko Caroline wote kutoka kampuni ya bia ya Serengeti ( SBL).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269