WALIMU waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani wakiingia kwa maandamano katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea ambapo Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete alikuwa mgeni rasmi na kuwahutubia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watoto waliomlaki muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa songea ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimnisho ya sherehe ya siku ya mwalimu duniani.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Samora mjini Songea mkoani Ruvuma akimkaribisha Rais Dr.Jakaya Kikwete kwa saluti maalumu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufungua rasmi jengo la Chama Cha waalimu mkoa wa Ruvuma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya mrisho kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la Chama Cha waalimu Tanzania Mkoa wa Ruvuma leo asubuhi mjini Songea.Wapili kushoto ni Rais wa Chama Cha waalimu Tanzania Bwana Gratian mkoba na watatu kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Maghembe.
Hivi tuseme ukweli upendo huo wa kushikana mikonoo utaendelea kuwepo hata baada ya kushinda na kuwa raisi...tuchukulie kama akishinda...sidhani hawa jamaa wa sare watakupa nafasi kweli!
ReplyDeleteHaya walimu nakilini hizo ahadi kwa `boll=pen' kama mtamchagua tena akipita msilalamike...muhakikishe mnakipata kile mlichoahidiwa...sijui kasema itachukua muda gani kuzipata hizo ahadi. Manake ahadi nyingine ni za ujanja, ana-ahidi lakini utekelezaji wake unaweza ukazidi miaka yake mitano...Tunataumai ahadi zinazotolewa na wagombea zitatolewa na kuanishwa kwa muda gani!