BENKI ya KBC (Tanzania ) Limited, imeipa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), msaada wa Sh. milioni 10 kwa ajili ya kuboresha maabara ya ugonjwa unaoathiri chembechembe nyekundu za damu 'sickle cell'. Pichani, Mkuu wa Huduma ya Maabara wa hospitali hiyo, Dk. Emmael Moshi (kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KBC iliyotoa msaada huo, JoramKiarie, leo mjini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KBC, Christina Manyenye. Msaada huo uliotolewa leo ni awamu ya pili baada ya ule wa awamu ya kwanza wa sh. milioni 7.3 uliotolewa na Benki hiyo mwaka 2008 kwa ajili ya kuboresha maabara hiyo. Kwa habari zaidi kuhusu KBC tembelea www.kcbbankgroup.com
Your Ad Spot
Oct 18, 2010
Home
Unlabelled
KBC YATOA MILIONI 1O KUBORESHA MAABARA YA 'SICKLE CELL' MUHIMBILI
KBC YATOA MILIONI 1O KUBORESHA MAABARA YA 'SICKLE CELL' MUHIMBILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269