Breaking News

Your Ad Spot

Oct 12, 2010

MGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA APANDISHWA KIZIMBANI KAWE

MGOMBEA udiwani kata ya Wazo, kwa tiketi ya CHADEMA,Joseph Msett (kuhsoto) akitia saini hati ya dhamana baada ya kupandishwa kizimbani leo  mahakama ya mwanzo Kawe kujibu shitaka la kutishia kuua kwa maneno.


Mgombea huyo anadaiwa kumtishia kumuua m,gombea wa nafasi hiyo, Livinus Gutambi, kupitia tiketi ya CCM.
Akisoma shitaka hilo, Koplo Elias Umbedo, alidai mbele ya hakimu Mfawiodhi wa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Sophia Mwaipopo kuwa, Oktoba 11,mwaka huu, saa 7.30 mchana, mshitakiwa alitenda kosa hilo.

Umbedo alidai kuwa kwa nia na makusudi mshitakiwa alimwambia mlalamikaji kuwa atamuua kwa sababu anasema vibaya katika mkutano wa kampeni. Mshitakiwa alikana shitaka ambapo upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages