Breaking News

Your Ad Spot

Oct 28, 2010

YALIYOJIRI LEO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, JUMAPILI HII

Waangalizi wa ndani na nje ya nchi wa uchaguzi mkuu wakiwa katika mkutano na Tume ya Uchaguzi zanzibar (ZEC), leo katika ukumbi uliopo Hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.  
Waangalizi wa uchaguzi mkuu wakitumia kompyuta kutuma taarifa zao kwa mtandao wa internet uliowekwa katika ukumbi maalum utakaotumika kutangaza matokeo na shughuli nyingine za uchaguzi huo, uliopo hoteli ya Bwawani, Zanzibar. 
Ukumbi huu ndio utatumika kutangaza matokeo ya Uchaguzi Zanzibar, una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 100. 
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi, Zanzibar (ZEC), Khatib Mwinchande, akizungumza, wakati wa mkutano wake na waangalizi wa uchaguzi mkuu, Zanzibar, leo katika ukumbi maalum uliopo hoteli ya Bwawani, Zanzibar 
Waangalizi wa uchaguzi mkuu waliopo Zanzibar, si tu wanafuatilia uchaguzi huo ila pia wanafanya utalii katika kisiwa hicho. Pichani, wakitembelea soko la Darajani. leo. 
Picha za wagombea Rais Kikwete (CCM-urais), Dk. Shein (Urais zanzibar-CCM), Profesa Lipumba (Urais-CUF) na Seif Sharif Hamad (urais zanzibar (CUF) ndizo pekee zinatawaka katika viunga mbalimbali vyenye vuguvugu la mambo ya siasa Zanzibar, huku mgombea wa Chadema anayechacharika Bara Dk. Wilibrod Slaa picha zake zikiwa hazipo kabisa katika maeneo hayo. Pichani, ni eneo la soko la Darajani. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages