Breaking News

Your Ad Spot

Oct 15, 2010

ZENGWE LA MADAI YA WAZEE WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI YA ZAMANI LACHACHAFYA TENA LEO BAADA YA SHAURI LAO KUAHIRISHWA MAHAKAMA KUU

Wadai wa mafao ya iliyokuwa Afrika Mashariki wakiwa nje ya mahakama kuu leo asubuhi, kusikilizia wakati shauri lao likiendelea ndani 
Kukaa kwa muda mrefu eneo hilo, kukatengeneza pia mazingira ya biashara. Hili ni kreti la soda zilizokuwa zikiuzwa kwa wastaafu hao ili wenye chochote waweze kupoza koo. 
Mama muuza mihogo naye akachangamkia fursa hiyo, hapa wananunua mihogo mibichi kuongeza wanga mwilini
Baada ya kupata jibu la kuahirishwa shauri lao, wakaamua kufunga barabara kwa kizuizi cha kanga zenye chapa ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere 
Baada ya kuziba barabara, vijana wanaofuatilia madai ya wazee wao, wakajitwisha jukumu la kuzuia wasafiri. hapa ni mmoja wa vijana hao akijaribu kumzuia JW mwenye pikipiki lakini hakufanikiwa. 
Halafu akataka kupita jamaa na Bajaji, lakini kwa kuwa hakuwa na ubavu kama huyo JW, kijana akaisukumiza kurudi nyuma bajaji hiyo isipite na akafanikiwa. 
Na hawa nao wakiwa katika pikipiki yao, wanashangaa kuona kijana akiweka kizuizi mbele yao ili wasipite, wakalazimika kugeuza pikipiki yao kutafuta njia nyingineBaadaye walitimuliwa na polisi kwa gari la maji ya muwasho 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages